Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  19 Shawwal 1443 Na: 1443 H / 22
M.  Alhamisi, 19 Mei 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

P.K. Halder ni Kikaragosi Kidogo katika Mchezo Muovu wa Urasilimali Msekula; ambapo Kifungo cha Jela ni Kinga kwa wengine kutokana na kuregesha Pesa Zilizoporwa

(Imetafsiriwa)

Mlaghai mtoro wa Bangladesh Prashanta Kumar Halder, anayejulikana pia kama P.K. Halder, alikamatwa eneo la Bengal Magharibi nchini India mnamo Mei 14, 2022 na Kurugenzi ya Utekelezaji Sheria ya India. Mhalifu huyu hatari P.K. Halder alikuwa mfanyakazi wa ngazi ya juu wa benki (Meneja Mkurugenzi wa zamani wa NRB Global Bank) na alisakwa nchini Bangladesh kwa ulaghai wa Taka bilioni 102 (dolari bilioni 12.03 za Marekani) kutoka kwa taasisi tofauti za fedha zisizo za benki (NBFIs) na kukusanya mali haramu nchini Bangladesh huku akizipenyeza zilizosalia hadi Canada, Singapore, na India. P.K. Halder ni sehemu ya utawala wa Hasina na vile vile mfumo wa utawala wa kisekula uliojengwa juu yake. Halder alikuwa mtu mwenye uhusiano wa karibu na utawala wa Hasina na hivyo angeweza kupata nyadhifa za juu katika taasisi kadhaa za kifedha ili kutumikia maslahi ya wanasiasa chini ya miaka kumi. Vyenginevyo, angewezaje kutorokea India licha ya marufuku ya Mahakama Kuu! Na kuregeshwa kwake Bangladesh na kesi iliyofuata itakuwa ni kutokujali sheria kwa kutorudisha pesa zilizoporwa kwani tayari waziri wa Hasina na Tume ya Kupambana na Ufisadi alikiri kwamba kukamatwa kwake kunaweza kusababisha kuregeshwa kwa pesa za watu. Kwa hivyo, licha ya vyombo vya habari kuongeza chumvi, watu hawana furaha kwani wanajua kwamba Halder hatimaye atakuwa huru kupitia mchakato wa kisheria wa kisekula.

Enyi Watu! Kumekuwa na wengi kama P.K. Halders ambao walifanya kazi kwa serikali na kufanya kashfa kubwa zaidi za benki moja baada ya nyingine katika miaka 10-12 iliyopita. Munashuhudia uporaji wa Taka bilioni 45 za Benki ya BASIC, huku mpangaji wake mkuu Sheikh Abdul Hye Bacchu, aliyekuwa mwenyekiti wa benki hiyo, akiwa bado hajaguswa hadi leo na wala hakusumbuliwa hata kidogo na ACC kutokana na uhusiano wake mkubwa na Sheikh Hasina. Muliona Taka bilioni 43.57 za Hallmark Group ikiiba kutoka Benki ya Sonali inayomilikiwa na serikali, Taka bilioni 34.43 kuporwa na Crescent Group kutoka Benki ya Janata, na Bismillah Group ikiiba Taka bilioni 12 kutoka kwa benki nne. Msururu wa uporaji wa mabenki wa mabilioni ya dolari sasa umewafanya watu kutojali habari za ulaghai wa Taka 100 au Taka bilioni 1, ambao unaendelea bila kupungua ndani ya muundo wa sheria. Kwa utawala wa kibepari wa kisekula wa Hasina unaonyonya damu, hata haya makashfa elfu moja ya crore si habari kubwa tena. Waziri wa zamani wa Fedha wa serikali ya Hasina AMA Muhith, mbunifu wa 'Maendeleo Makubwa' ya serikali ya Hasina, alisema baada ya kashfa mbaya ya mkopo wa Benki ya Hallmark-Sonali kwamba ulaghai wa mkopo wa Taka bilioni 30 hadi Taka bilioni 40 sio jambo kubwa kwa uchumi wetu! Ukweli ni, watu walikuja kufahamu kuhusu uporaji huu wa utaratibu wa benki wakati mmoja wa wakopeshaji wakubwa wa benki waliosusia kulipa mkopo nchini humo Salman F Rahman, ambaye alifungwa kwa ulaghai mwaka 2007-8, aliteuliwa kuwa mshauri wa masuala ya kiuchumi wa Waziri Mkuu Sheikh Hasina miaka michache nyuma, na sasa ni waziri. Serikali ya Hasina hapa inafuata mkakati wa pande mbili kuendeleza ufisadi. Inachagua kuwaandama na kuwakaanga samaki wadogo ilhali inawacha programu ya uporaji kuendelea kufanya kazi kupitia kuwaruhusu wababe kuwa huru. Lakini PK Halder na mithili yake pia wanatuzwa na pote la ubepari kwa kujitolea kwao katika kamari hii. Anajua fika kwamba kukamatwa kwake kwa kweli ni kinga ya yeye kutoroka pamoja na mali nyingi bila kujeruhiwa. Hatimaye, atatoka jela bila ya dhima yoyote ya kurudisha pesa zilizoporwa.

Enyi Watu! Ingawa utawala wa Hasina "usiohimili hata kidogo" tayari ni bingwa wa ufisadi, tawala zingine za kisekula na vyama vya kisiasa pia hazina tofauti. Kwa sababu ufisadi umefumbatwa ndani ya itikadi ya usekula, haina viwango vya maadili na huzalisha ulafi wa mali kwa kila mwanadamu, achilia mbali kipote cha wafisadi. Kwa hivyo, ufisadi ni sifa kuu miongoni mwa kipote cha mabepari na wanasiasa wa kisekula sio tu nchini Bangladesh bali pia kote ulimwenguni.

Enyi Waislamu wa Bangladesh! Msivumilie mfumo huu unaowalisha mafisadi kupora pesa na rasilimali zenu zaidi. Msihadaiwe kwa kukamatwa kwa vikaragosi vidogo kama P.K. Halder kwani kukamatwa kwao hakudhamini kurudishwa kwa pesa zenu zilizoporwa. Wakati tatizo ni mfumo wenyewe wa kisekula wa kirasilimali, mnawezaje kutafuta suluhisho kutokana nao? Ili kukomesha ufisadi, lazima muinuke ili kuuondoa mfumo muovu wa kirasilimali na kuiregesha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume iliyoahidiwa. Hakutakuwa na nafasi ya kupewa muamala maalum kwa vipote fulani ndani ya Khilafah, na wala walaghai na mafisadi hawatapata njia yoyote ya kustawi humo. Shariah ya Kiislamu kamwe haivisazi vipote kwa ufisadi wao, badala yake huwapa faraja masikini kwa kusimamisha kwa muda adhabu wakati wowote wa janga. Mtume (saw) aliamuru kukata mkono wa mwanamke wa kabila tukufu la Makhzumi la Kiquraishi kwa ajili ya wizi, ambapo yeye (saw) alisema kwamba «لَا قَطْعَ فِي مَجَاعَةِ مُضْطَرٍّ» “hakuna kukata (mkono) wakati baa la njaa” (imepokewa na al- Sharkhasi katika al-Mabsut) kuwapa afueni masikini na mafukara. Kwa hivyo, jiungeni na mapambano ya kisiasa ya kusimamisha tena Khilafah Rashida chini ya uongozi wa Hizb ut Tahrir ili kuhakikisha usawa na kuwazuia watu wasishawishike kuongeza mali zao kupitia wizi au ulaghai.

 Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu