Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  25 Rabi' II 1442 Na: 1442 H / 12
M.  Alhamisi, 10 Disemba 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Uhamishwaji kwa Lazima wa Waislamu wa Rohingya kwenda Bhashan Char Kunafichua Sura Mbaya ya Utaifa

Katikati ya uwepo wa usalama mzito, serikali ya Hasina isiyo na huruma imeanza uhamishaji kwa lazima maelfu ya wakimbizi wa Rohingya katika kisiwa kilichotelekezwa na chenye kukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara, Bhashan Char, katika Ghuba ya Bengal. Waislamu mia tatu wa Rohingya ambao wametengwa kwenye ardhi hiyo isiyo salama mnamo Mei iliyopita tayari wako katika hali mbaya. Wanaume, wanawake na hata watoto walitandikwa kwa fimbo na maafisa wa usalama huko baada ya kugoma kula miezi michache iliyopita kwa ajili ya hali nzuri za kimaisha ("Rohingya wawashutumu maafisa wa Bangladesh kwa unyanyasaji juu ya mgomo wa njaa", Al Jazeera, 8 Oktoba 2020). Kwa hivyo, Bhashan Char kimsingi ni 'kambi ya uzuizi' ambapo wakimbizi Waislamu wataamiliwa kama wanyama. Sio tofauti na magereza ya uliokuwa ukoloni wa Kiingereza (Kala Paani au 'maji meusi') katika Visiwa vya Andaman na Nicobar, vilivyokuwa vikitumiwa kuwafunga maisha na kuwaadhibu wapinzani.

Waislamu wasio na wasimamizi wa Rohingya wameangukia kuwa waathiriwa wa siasa chafu za serikali ya Hasina. Hapo awali, serikali ilikuwa ikiwazuia wakimbizi wa Rohingya waliokimbia mauaji nchini Myanmar mnamo 2016. Lakini kwa kuogopa hamasa za Waislamu nchini Bangladesh, ililazimika kuwaruhusu waingie. Baadaye, ingawa imekuwa ikipora pesa zinazoitwa misaada inayokuja kwa jina la Waislamu wa Rohingya ilhali ikiwatia ndani ya kambi mbaya zinastahiki wanyama, serikali hii ya kisekula imekuwa ikitia kwa busara na polepole fikra za sumu dhidi ya Waislamu hao wanyonge katika jamii. Kwa upande mmoja, wanaume wa chama tawala wamekuwa wakitumia vibaya taabu zao na kuwalazimisha kufanya uhalifu wakati wa unyanyasaji wao. Kwa upande mwingine, serikali ya Chanakya Hasina imekuwa ikitumia wasomi wa kupe na vyombo saliti vya habari kusababisha hofu na uhasama dhidi ya wahasiriwa hawa ili kuhalalisha kuhamishwa kwao hadi kisiwa hicho kisichoweza kufikika ambacho jina lake, Bhasan Char, linamaanisha 'kisiwa kilichojaa maji'. Wasiwasi wa kiuchumi na ghariza za kuhifadhi maisha za watu wa Bangladesh zinazalishwa kwa hila, haswa wakati wa hali hii ya Covid-19, kwa kudai kwamba watu milioni 1 hawa watasababisha upungufu wa chakula na shida za ajira katika idadi ya watu milioni 200! Kana kwamba miongo kadhaa ya utawala mbaya na uporaji wa pesa na rasilimali za watu na serikali za kisekula haijatutosha kuteseka shida za kijamii na kiuchumi! Kwa hivyo, ni dhahiri kwamba huku watu wa Bangladesh wakiwa wamechoshwa na utawala wa kisekula, serikali ya Hasina inajaribu kulinda mipaka yake kwa kupanda nyuma ya utaifa uliooza. Ni kwenda kinyume na amri ya Mwenyezi Mungu (swt):

[وَاِنِ اسۡتَـنۡصَرُوۡكُمۡ فِى الدِّيۡنِ فَعَلَيۡكُمُ النَّصۡرُ]

“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia.” [Surah Al Anfal: 72] na kujaribu kutenganisha hisia zozote za kidugu au ubinadamu katika watu wetu kuhusu "wakimbizi" hawa. Kwa kisingizio cha uongo cha utaifa, serikali inajaribu kuwafanya watu wasahau kuwa hawa ni Waislamu wanaohitaji, na hata kwamba kulikuwa na wakati ndani ya nyakati zetu nyingi za maisha wakati watu milioni 10 walidaiwa kuwa wakimbizi katika nchi nyingine. Pia hatuwezi kupuuza ukweli kwamba kwa kuingiza kwa makusudi chuki dhidi ya Waislamu wa Rohingya katika damu ya kisiasa ya Waislamu nchini Bangladesh, serikali ya Hasina inajaribu kuenzi urithi wa kikoloni wa "Gawanya na Utawale" kutimiza ajenda ya mabwana zao wa Magharibi kudumisha mgawanyiko wa Ummah huu kupitia mipaka batili ya kitaifa iliyowekwa na wakoloni na wakubali kutelekezwa kwa ndugu na dada zao Waislamu waliodhulumiwa.

Enyi Waislamu, pingeni njama hii ya serikali ya kisekula ya Hasina ya kuingiza sumu ya utaifa katika akili zetu. Fikra hii ovu huzaa unyama na itatumika kuhalalisha uhamisho wa lazima wa ndugu na dada zetu wanaoteswa. Watawala wetu wa serikali za kitaifa wanawaonyesha wahasiriwa hawa kama wahalifu wa kigeni na kuwasha chuki dhidi yao kwa sababu tu wametoka nchi tofauti, wakati watawala wa kisekula na wanaume wa chama tawala wao ndio wanapaswa kutengwa katika kisiwa hicho kwa uhalifu wao endelevu na usaliti. Watawala hawa wasaliti watatumia kila zana ili kutufanya tugawanyike kikabila, na kimaeneo ya kijiografia kwa kuwatumikia mabwana zao wa kikoloni wa Magharibi haswa kwa kuwa mabwana zao wanaogopa juu ya kurudi hivi karibu kwa Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume iliyoahidiwa  .

Enyi Waislamu, jihadharini! Ikiwa huwezi kuzikomboa akili zenu kutokana na minyororo na maradhi ya fikra za kitaifa na kupambana kusimamisha tena Khilafah, ngao pekee na msimamizi wa Waumini na wanaodhulumiwa, tutamjibuje Mwenyezi Mungu al-Haseeb (Mhisani wa Waja) pindi tutapoulizwa juu ya matendo yetu kwa wanawake na watoto waliokata tamaa wakati walipoomba msaada wetu? Mtume (saw) amesema,

«الْمُسْلِمُ أَخُو الْمُسْلِمِ، لَا يَظْلِمُهُ، وَلَا يَخْذُلُهُ»

“Muislamu ni ndugu ya Muislamu, hamdhulumu, wala hamtelekezi.”

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu