Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Ewe Waziri Mkuu wa Malaysia! Kumfuata Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) si kwa Maneno tu, bali ni kwa Moyo na Vitendo

Ni wajibu kwa yeyote anayetamani Madina kuwa kama nchi kigezo cha kuigwa kufanya kazi kwa umakini kwa ajili ya kusimamisha tena Dola ya Kiislamu (Khilafah). Dola hii ya kupigiwa mfano mwanzoni iliasisiwa na Mtume (saw), baadaye ilishikiliwa na Khulafa'ar-Rashidin, Umawiyya, Abbasiyya, na Uthmaniyya, na kisha ikavunjwa rasmi mnamo tarehe 28 Rajab 1342 H (sawia na tarehe 3 Machi 1924 M). Muundo huu hautahuishwa tena kupitia matamshi ya viongozi au maneno tu; bali inahitaji imani, na juhudi za kujitolea na za dhati kutoka kwa wale wote wanaoitetea.

Soma zaidi...

Uchaguzi ni Njia ya Kuendeleza Mfumo wa Kisekula ambao lazima Ubadilishwe kwa Kusimamisha Khilafah

Tangu kuzuka mapinduzi ya Umma nchini Tunisia mwishoni mwa mwaka 2010, Hizb ut Tahrir imesisitiza kuwa mradi pekee wa kihadhara wenye uwezo wa kuyafanikisha mapinduzi hayo na kufikia matakwa ya wanamapinduzi unatokana na kuupindua utawala wa kisekula na badala yake kuubadilisha kwa mfumo adilifu wa kisiasa, na hili linaweza tu kufanywa kupitia Uislamu, chini ya dola moja; dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Soma zaidi...

Barua ya Wazi kwa Watu Wenye Nguvu katika Majeshi ya Waislamu Kutoka kwa kina Mama, Dada na Mabinti wa Ummah wa Kiislamu ili Kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina

Huu ni ujumbe kwa ndugu zetu, baba zetu na watoto wetu wanyoofu katika majeshi ya nchi za Kiislamu kutoka kwa wanawake wa Umma huu mtukufu wa Kiislamu. Tunakuhutubieni kama wale ambao wamepewa wajibu na Mola wa Walimwengu wote (swt) kuwalinda Waislamu na kulinda heshima yetu. Tunakuhutubieni kama watu wenye uwezo wa kukomesha mauaji ya Ummah wetu.

Soma zaidi...

Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kinachapisha Barua ya Wazi kwa Majeshi ya Waislamu ili Kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina

Takriban watu 40,000 wameuwawa mjini Gaza katika kipindi cha miezi 10 iliyopita, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, huku serikali za ulimwengu, zikiwemo nchi za Waislamu zikitazama kama watazamaji pekee wa mauaji haya ya umwagaji damu, bila ya dhamira yoyote ya kisiasa ya kukomesha mauaji hayo. Hakika, tawala nyingi za ardhi za Kiislamu kwa miongo kadhaa zimeimarisha mkono wa uvamizi wa Kiyahudi kupitia mikataba yao ya amani, kuhalalisha mahusiano ya kidiplomasia, na ushirikiano wa kiuchumi na umbile hili la mauaji ya halaiki.

Soma zaidi...

Majeshi ya Waislamu Yanasukumwa na Marekani Popote Inapotaka, Lakini Hayasukumwi na Uungwana wa Al-Mu'tasim!

Kanuni msingi ya majeshi ya Waislamu ni kwamba wabebe Aqida ya Kiislamu (itikadi); ipasavyo, haijuzu kwao kuchukua hatua yoyote mpaka wajue hukmu ya Mwenyezi Mungu kuhusu hilo. Lakini kwa bahati mbaya wamejisalimisha kwa watawala wasaliti na vibaraka, wakitii amri zao na kutekeleza maamuzi yao hata wakiwa katika ghadhabu ya Mwenyezi Mungu.

Soma zaidi...

Udungaji Visu Mgongoni mwa Umma Unaendelea kutoka kwa Watawala Vibaraka Ruwaibidha wa Waislamu!

Ufalme wa Al Saud unaregesha udungaji visu wake mgongoni mwa Umma wa Kiislamu kwa kushirikiana na watawala wa Ruwaibidha (watepetevu na wazembe) katika nchi za Kiislamu kupitia mbio zao za kuhalalisha mahusiano na umbile nyakuzi, licha ya jinai zote za mauaji ya halaiki na uhangaishaji Waislamu katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi unaofanywa na umbile hilo katili.

Soma zaidi...

Marekani Yazipatia India na Umbile la Kiyahudi Silaha za Kisasa, Huku Ikiweka Vikwazo kwa Mpango wa Makombora ya Ballistiki wa Pakistan

Sera ya Marekani kwa Ulimwengu wa Kiislamu ni sera ya kuwatiisha na kuwadhalilisha Waislamu, kwa kuungwa mkono na kuwatia nguvu maadui wa Ummah. Kuhusu Pakistan haswa, Marekani inataka kuidhoofisha Pakistan ili kuruhusu India kuinuka, ili Dola hiyo ya Kibaniani iweze kukabiliana na Waislamu na China kwa niaba yake.

Soma zaidi...

Tunahitaji Sana Khilafah Kuilinda Bahari ya China Kusini

Mgogoro wa Bahari ya China Kusini umeibuka tena kufuatia kuvuja kwa waraka wa kidiplomasia kutoka Jamhuri ya Watu wa China (PRC) kwa Ubalozi wa Malaysia jijini Beijing, wa tarehe 18 Februari. Ujumbe huo ulifichua pingamizi ya China na kuitaka Malaysia kusitisha shughuli za utafiti wa mafuta na gesi huko Beting Raja Jarum na Beting Patinggi Ali, maeneo ya ndani ya Visiwa vya Spratly.

Soma zaidi...

Watoto wa Palestina Watakuwa Mahasimu wa Ummah na Majeshi Yake Siku ya Kiyama iwapo Hawatasonga Kuwanusuru

Msichana mwenye umri wa miaka 13, Bana Amjad Bakr, aliuawa shahidi baada ya kupigwa risasi kifuani na wanajeshi wavamizi jioni ya Ijumaa, Septemba 6, 2024, wakati wa shambulizi la walowezi, wakisaidiwa na vikosi vya uvamizi, kwa kijiji cha Qaryut, kusini mwa Nablus katika Ukingo wa Magharibi.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu