Kitengo cha Wanawake cha Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Chafanya kwa Mafanikio Kongamano la Kimataifa la Wanawake Mtandaoni “Ukombozi wa Palestina... Changamoto na Bishara Njema”
- Imepeperushwa katika Kitengo cha Wanawake Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kitengo cha Wanawake cha Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, kwa uratibu na wanawake wa Hizb ut Tahrir kote ulimwenguni, kilifanya kongamano la kimataifa la wanawake mtandaoni lenye mafanikio kwenye jukwaa la Zoom kwa kichwa “Ukombozi wa Palestina: Changamoto na Bishara Njema” mnamo siku ya Jumamosi, Oktoba 5, 2024. Mamia ya wanawake wanaozungumza Kiarabu kutoka kote duniani walihudhuria kongamano hilo, katika ukumbi wa mikutano na kwenye kurasa za Facebook za Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir. Wazungumzaji kutoka Palestina, Tunisia, Syria, Lebanon, Indonesia na Amerika walishiriki katika kongamano hilo.