Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  19 Rabi' II 1440 Na: 1440/009
M.  Jumatano, 26 Disemba 2018

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Majibu kwa Uzushi wa Dar al-Ifta ya Misri
(أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّهِ حُكْماً لِقَوْمٍ يُوقِنُونَ)
“Je, ni hukumu za kijahiliya ndizo wanazozitaka? Na nani mbora zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini”
(Imetafsiriwa)

Uislamu umelitambua jambo la ijtihad, ambapo Mujtahid anatia juhudi yake kuvua hukumu ya kifiqhi ya kivitendo kutoka kwa dalili zake fafanuzi katika machimbuko ya sheria na kuipachika juu ya uhalisia wa mada (Manat) ya hukumu hiyo. Ni dhahiri, Ijtihad haifanywi katika mambo yaliokatikiwa (Qati’), bali katika mambo yasio na mkato (Dhanni), na hivyo basi Mujtahid hupokea ujira mara mbili anapofanya Ijtihad na akapata, na hupokea ujira mmoja endapo atakosea katika Ijtihad hiyo. Ijtihad haikufungwa kwa mtu au chama, bali ni kwa wale wote walio na uwezo wa kufanya Ijtihad.

Hivyo basi, cha kushangaza ni ripoti iliyotolewa mnamo 12/12/2018 na ule unaoitwa “Muongozo wa Fatwa wa Kiulimwengu”, unaotayarishwa na kitengo cha masomo ya kimikakati katika Dar al-Ifta ya Misri (Jumba la Fatwa), kwa anwani “Fatwa juu ya miamala ya kiuchumi katika mashirika ya kigaidi” (uliochapishwa katika tovuti ya Dar Al-Ifta (http://dar-alifta.org.eg/AR/Viewstatement.aspx?sec=media&ID=6205). Ikiwa Dar al-Ifta imeenda kinyume na Ijtihad nzito, na kuwasilisha hukumu tofauti kwa msingi wa ufahamu sahihi zaidi na sawa zaidi ya maumbile ya mada (Manat), au kwa msingi wa dalili nzito ya kifiqhi, ingekubaliwa kuwa na mjadala kwayo. Lakini, Dar al-Ifta ya Misri baada ya kutafuta kwa takriban saa 90 pamoja na wataalamu na wajuzi, inakuja na fatwa ya kuharamisha sarafu ya bitcoin na kisha kunukuu fatwa kama hiyo iliyotolewa na Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa, Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah, Allah amuhifadhi, na inaikashifu Hizb kwa kuharamisha sarafu ya bitcoin, “Miongoni mwa vitu ambavyo Hizb ut Tahrir inaharamisha ni “Bitcoin” kwa mujibu wa fatwa ya Amiri wake ambayo inajumuisha: “Sarafu ya Bitcoin sio pesa; haikadiriwa kama pesa katika sharia’h ya Kiislamu, kama ilivyo wazi kwa muamala usio hakika au bidhaa isiyo julikana (majhool),kwa hivyo hairuhusiwi kuinunua au kuiuza.”” Hivyo basi, hatuelewi kuna nini hapa?! Na ni upi upinzani wa Dar al-Ifta ya Misri!!!   

Lakini baada ya kuangalia uhalisia wa huu “Muongozo wa Fatwa wa Kiulimwengu” na ni nani aliye nyuma yake, tunapata kuwa si chengine zaidi ya kuwa ni mojawapo ya ala za Dar al-Ifta ya Misri, iliyoapa kwenda kinyume na njia ya Mwenyezi Mungu na kuitetea serikali ya kihalifu nchini Misri, huku Amerika, kinara wa ukafiri na firauni wa zama hizi, ikiipa uwezo juu ya nchi hiyo na shingoni mwa watu wake, ikiweka ukutani mwake sanamu lake tukufu kwa jina “demokrasia” inayompiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake kupitia kuwatungia watu sheria, yaani kuhalalisha au kuharamisha, badala ya Mola wa watu, na Amerika inalingania sanamu hili na kuzisifu chaguzi chini yake. Lakini, watu wa Misri walipomchagua Dkt. Mohamed Morsi kama mtawala wao, kupitia uchaguzi wa “kidemokrasia”, Amerika haikuunga mkono kuendelea kwa utawala wake, lakini ikaamua kumbandikiza mtumishi wake Sisi kuwatawala watu kupitia ukandamizaji, uimla na fikra ya kifirauni. Muongozo wa Fatwa wa Kiulimwengu si chengine isipokuwa ni pazia ambayo Amerika inajificha nyuma yake ili kudhibiti hatima ya nchi hiyo na watu katika ardhi hiyo ya Kinanah.     

Ndio, ni Sisi mwenyewe ambaye amekariri kusema kuwa wanazuoni wa Al-Azhar wanapaswa kufanya mapinduzi ya kidini, sio ya kuikomboa nchi hiyo kutokana na uchafu wa Amerika na kuwaongoza wanajeshi jasiri wa Kinanah ili kuikomboa Al-Aqsa Tukufu, Qibla cha kwanza cha Waislamu na Masra (mahali pa safari ya Isra) ya Mtume wao Mtukufu kutokana na uchafu wa Mayahudi, bali kukabiliana na “Uislamu wenye misimamo mikali” kwa madai yao fisidifu.

 (وَإِنَّ مِنْهُمْ لَفَرِيقاً يَلْوُونَ أَلْسِنَتَهُم بِالْكِتَابِ لِتَحْسَبُوهُ مِنَ الْكِتَابِ وَمَا هُوَ مِنَ الْكِتَابِ وَيَقُولُونَ هُوَ مِنْ عِندِ اللَّهِ وَمَا هُوَ مِنْ عِندِ اللَّهِ وَيَقُولُونَ عَلَى اللَّهِ الْكَذِبَ وَهُمْ يَعْلَمُونَ)

“Na wapo baadhi yao wanaopindua ndimi zao katika kusoma Kitabu ili mdhanie kuwa hayo yanatoka Kitabuni, na wala hayatoki Kitabuni. Na husema: Haya yametoka kwa Mwenyezi Mungu. Na wala hayatoki kwa Mwenyezi Mungu. Na wanamsingizia Mwenyezi Mungu urongo ilhali wao wanajua.” [Aal-Imran: 78]

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya muongozo: “Kama ilivyo simamiwa na Muongozo wa Fatwa wa Kiulimwengu, chama hiki kimetabanni kwa asilimia 100 shutuma kwa serikali zilizopo na uchumi wao katika muundo wa udadisi unaotolewa na Amiri wa chama hiki, ya dhahiri zaidi ni maoni yake juu ya hali ya uwekezaji nchini Sudan, akisema: “Sio lengo la kampuni za kikoloni za kirasilimali kutatua tatizo la ukosefu wa ajira au ajira kwa wafanyikazi wenyeji. Suluhisho msingi kwa matatizo ya uchumi ni kusimamisha dola kwa msingi wa Uislamu.” Hivyo basi, katika dini ya firauni mpya wa Kiamerika, kukashifu serikali vibaraka za firauni huyo wa zama hizi na kutaka kuasisiwa kwa dola kwa msingi wa Uislamu ni fedheha, ambapo, kutusi umbile la kiwahyi na kutoa wito wa kuvuruga utekelezwaji wa Quran hadharani kwao wao ni uhuru wa rai unaodhaminiwa na dini yao, Mwenyezi Mungu awaangamize; wamedanganyika kiasi gani!   

Na hili kwa yakini linafafanua ukavu wa warongo hawa ambao wananukuu tarakimu zilizotolewa na ujasusi wa Amerika juu ya waathiriwa wa mashambulizi yanayodaiwa kuwa ya “kigaidi” nchini Afghanistan na Syria, huku maelfu ya waathiriwa wa Kiislamu waliouwawa kutokana na uhalifu wa Kiamerika, ima moja kwa moja mikononi mwa Waamerika nchini Afghanistan au kupitia kibaraka wao mmwagaji damu wa Damascus Bashar nchini Syria, au kupitia kibaraka wao al-Maliki nchini Iraq, au kupitia Sisi nchini Misri Kanana …ambao wote “Muongozo wa Fatwa wa Kiulimwengu” kamwe haujawasikia au labda umewasikia lakini ukaona aibu kuyabariki mauaji yao!

Si ajabu kuwa wachawi hawa wa Firauni wanautambua ulinganizi wa Hizb ut Tahrir wa kusimamisha dola ya Khilafah kwa njia ya Utume ili kutekeleza sheria ya Mwenyezi Mungu, na wala sio sheria ya Amerika na Wamagharibi makafiri. Ndio maana si ajabu kwamba wanauchukulia wenye kuharibu dini ya Amerika na utumwa wake unaolazimishwa juu ya Waislamu. Ummah huu, ambao umekirimiwa na Mwenyezi Mungu Ta’ala kama Ummah bora kutoka kwa watu, unao amrisha mema (al-Ma’roof) na kukataza maovu (al-Munkar). Jema la kwanza ni kuwalingania watu kumuabudu Mwenyezi Mungu mmoja wa pekee na kutangaza kumpwekesha Kwake kupitia kujisalimisha katika maagizo na makatazo Yake, na ovu la kwanza ni kujisalimisha katika hukumu ya Kikafiri (al-Taghut) yoyote iwayo na kwa majina yoyote yale.    

 (أَفَغَيْرَ دِينِ اللَّهِ يَبْغُونَ وَلَهُ أَسْلَمَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعاً وَكَرْهاً وَإِلَيْهِ يُرْجَعُونَ)

“Je, wanataka dini isiyo kuwa ya Mwenyezi Mungu, na hali kila kilichomo mbinguni na katika ardhi, kimesilimu kwa kumt'ii Yeye kikipenda kisipende, na kwake Yeye wataregeshwa?” [Aal-Imran: 83].

Tunatamatisha kwa kuwaambia wachawi wa Amerika kwamba kwa yakini Mwenyezi Mungu atatimiza ahadi Yake ya kweli:

 (يُرِيدُونَ لِيُطْفِئُوا نُورَ اللَّهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَاللَّهُ مُتِمُّ نُورِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ)

“Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru Yake ijapo kuwa makafiri watachukia* Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake (Muhammd (saw)) kwa uongofu na Dini ya Haki (Uislamu), ipate kushinda dini zote ijapo kuwa washirikina watachukia.” [At-Tawba: 32-33]

Dkt. Osman Bakhach
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.domainnomeaning.com
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) domainnomeaning.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu