Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  14 Shawwal 1445 Na: Afg. 1445 H / 15
M.  Jumanne, 23 Aprili 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hakuna Utiifu kwa Kiumbe katika Kumuasi Muumba!

(Imetafsiriwa)

Idara ya Ujasusi ya Mkoa wa Kandahar inawazuia wabebaji Da’wah kadhaa wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Afghanistan kwa miezi 12 iliyopita. Wiki hii, imefikia kipindi chake cha mwaka mmoja. Mbali na kuteswa na maafisa wa ujasusi, wamekuwa korokoroni bila hukumu kutoka kwa mahakama wakati huu. Mbali na hilo, maafisa hao wa ujasusi wa Kandahar wamewaambia wabebaji Da’wah hao kwamba ima waachane ulinganizi wa Khilafah au watateseka kutokana na shida na kifungo kwa muda usiojulikana.

Afisi ya habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Afghanistan inazingatia kuangazia nukta zifuatazo kuhusu tukio hili:

Kwanza, tumeshtushwa na vitendo kama hivyo vya maafisa wa ujasusi wa Kandahar. Je, kitendo/hoja kama hizo zimevuliwa katika dhehebu (Madh’hab) au Sharia gani? Uislamu ambao tunaufahamu unapinga wazi hatua kama hizo. Madai kwamba wabebaji Da’wah wamefungwa kwa sababu ya ukiukaji wao wa maagizo ya serikali na amri ya Amiri ni hoja isiyo na msingi. Hakuna amri iliyoandikwa na Amiri wa serikali ya sasa kuhusu marufuku ya Da’wah ya Hizb ut Tahrir. Mbali na hilo, maafisa wa ujasusi wa Kandahar wamekuwa wakikataa kabisa kutekeleza amri wazi na/au maagizo yaliyotangazwa na Amiri wa serikali kama "kuzuia kuwekwa kizuizini kwa watu wasio na hatia", "kuzuia adhabu bila hukumu ya mahakama", "kuzuia kuadhibu au kutesaa wakati wa uchunguzi ", na "kukabidhi kesi hizo kwa mahakama baada ya uchunguzi wa siku 10". Ikiwa kweli hili ni suala la kutotii na kukiuka amri ya Amir, basi kuna tofauti gani kati ya wafungwa na maafisa wa ujasusi ambao wenyewe wamekuwa wakikiuka Amri ya Amiri wao? Wanawaweka watu kizuizini kwa kudai kuhalifu amri zao na ilhali wao wenyewe wanawatesa watu, wanawaweka kizuizini watu bila ya utaratifu halali, ambayo hayo yako wazi dhidi ya amri za zilizotolewa kutoka juu kabisa.

Pili, Khilafah ndio taji la faradhi zote na jitihada za kuisimamisha ni wajibu wa kila Muislamu. Ikiwa mtu yeyote atatafiti na kuisoma Qur'an Tukufu, Sunnah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), makubaliano ya Maswahaba na hata maneno ya Maulamaa wa zamani, atapata kuwa hakuna kitu muhimu zaidi kuliko kusimamishwa kwa Khilafah. Kwa sababu hii, hakuna mtawala na/au kamanda wa jeshi anayeweza kuzuia wabebaji Da’wah kutekeleza wajibu huu, kugongana na amri ya Mwenyezi Mungu (swt) na ile ya Mtume (saw). Kama ambavyo mtawala hawezi kukataza Waislamu kuswali, kufunga, kutoa zakat na kuhudhuria jihad; Vivyo hivyo, hawezi kuwakataza Waislamu kutokana na faradhi ya kuamrisha mema na kukataza maovu na kitendo cha kuhakikisha kwamba watawala wanawajibika au kutokana na kubeba Da’wah ya Kiislamu. Kwani Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) wanataja:

[وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِالْمُنكَرِ وَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ]

“Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa.” [Aali-Imran:104]. «والَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، لَتَأْمُرُنَّ بالْمَعْرُوفِ، ولَتَنْهَوُنَّ عَنِ المُنْكَرِ، أَوْ لَيُوشِكَنَّ اللَّه أَنْ يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ جِعِقَابًا مِنْهُ، ثُمَّ تَدْعُونَهُ فَلا يُسْتَجابُ لَكُمْ» “Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake! Hamtaacha kuamrisha mema na hamtaacha kukataza maovu, isipokuwa Mwenyezi Mungu atakaribia kuteremsha juu yenu adhabu kutoka kwake, kisha mtamuomba wala dua zenu hazitajibiwa.”

Hivi sasa, wakati wabebaji Da’wah wa Hizb ut Tahrir wanatekeleza faradhi ya kuamrisha mema na kukataza maovu kwa ulinganizi wa kusimamisha Khilafah, je! Serikali tawala inachukulia kitendo hiki kuwa ni haramu licha ya nususi zilizotajwa hapo juu? Je! Inazingatia wabebaji Da’wah kuwa wanastahili kifungo, adhabu na kuteswa kwa sababu ya kutotii kwao serikali?! Ingawa, hakuna amri ya wazi kuhusu kuzuia ulinganizi wa kuregesha Khilafah ya Amiri wa serikali tawala; Lakini hata ikiwa ipo, haipaswi kutiiwa kulingana na Hadith ifuatayo, «لاَ طَاعَةَ لِمَخْلُوقٍ فِي مَعْصِيَةِ الْخَالِقِ» Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba!

Kwa msingi wa Hadith hii tukufu na iliyobarakiwa, katika historia yote, Maulamaa wa kidini kama vile Imam Abu Hanifa, Imam Ahmad bin Hanbal, Imam Shafi'i (Mwenyezi Mungu awawie radhi) na Maulamaa wengine kadhaa hawakutii maagizo ya haramu na/au amri za Khalifa halali wa zama zao – mpaka kufikia kiwango ambacho Khulafaa' (Makhalifa) sio tu waliwatia gerezani lakini pia waliwatishia kwa kifo. Lakini hofu ya watawala haikuwazuia kusema maneno ya haki. Kama vile kuteswa na kufungwa kwa Imam Ahmad bin Hanbal (Mwenyezi Mungu amuwie radhi) na Khalifa Mu’tasim kutokana na kupinga kwake 'nadharia ya kuumbwa kwa Quran Takufu' inajulikana vyema katika historia; Vivyo hivyo, hairuhusiwi kuwatii wanadamu kwa vitendo ambavyo husababisha kumuasi Mwenyezi Mungu (swt).

Mamlaka za serikali ya sasa hazipaswi kuchukua qiyas kati ya Hizb ut Tahrir na vile vyama vingine vya kimadhehebu ambavyo vimetokana kipekee na msingi wa miegemeo ya kikabila, dhehebu, lugha na nasaba - vile ambavyo vimechangia katika mgogoro na mgawanyiko wa kindani nchini Afghanistan. Hizb ut Tahrir ni chama cha kifikra na kisiasa ambacho kimekuwa kikijitahidi kusimamisha Khilafah kwa Ummah wa Kiislamu ambayo kwayo Uislamu utatabikishwa ili kuhakikisha kuwa ardhi zote za Kiislamu zinaungana tena. Hizb ut Tahrir kamwe haitaki Khilafah ili kupata malengo ya kichama; Badala yake, inataka kurudi kwa heshima na utukufu wa Waislamu wote. Kwa hivyo, tunawaonya maafisa wa ujasusi wa Kandahar kwamba unyanyasaji na kuteswa kwa wabebaji Da’wah wa Khilafah utasababisha ghdhabu ya Mwenyezi Mungu (swt), kwa hivyo acheni kufanya vitendo kama hivyo vya kihalifu na visivyo vya Kiislamu.

[وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ مُنقَلَبٍ يَنقَلِبُونَ]

“Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka.” [Ash-Shuraa’: 227]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu