Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hii ni Taarifa kwa Watu

Wito kwa Watu wa Tunisia, Ardhi ya Al-Zaitouna ya Vyuo Vikuu Vikongwe Ulimwenguni

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنْفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَاراً وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ]

“Enyi mlio amini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe.” [Surat At-Tahrim:6]
(Imetafsiriwa)

Tangu ukoloni ulipoingia Tunisia, ulilenga elimu na athari yake katika kuunda shakhsiya. Kwa hivyo mwanaorientalisti wa Ufaransa Louis Maigret alichukua jukumu la elimu ya umma nchini Tunisia, akipendekeza mradi wa kielimu unaolenga kuidhibiti zaidi nchi na watu wake kielimu na kisiasa. Hili lilifanikiwa kwa kutoa mafunzo kwa kipote cha wasomi wa Tunisia waliojaa thaqafa ya Kimagharibi, wakishikamana na mtaala wa lugha ya Kifaransa na usekula.

Kisha, vikosi vya wakoloni viliondoka baada ya kuhakikisha uwakilishaji wa watawala kwao na miradi yao. Bourguiba alitabanni Mradi wa Ufaransa wa Mageuzi ya Elimu wa Jean Debiessefor (kama alivyodai). Mahmoud El Materi, Waziri wa la Elimu ya Kitaifa, alipewa jukumu kuanzia Januari 1958 la kusuka mitaala ya elimu ndani ya mipaka ya muundo wa Ufaransa na kutekeleza mpango wa Mfaransa Jean Dubois, ambaye aliieleza lugha ya Kiarabu kama "iliyo na mapungufu na haifai kutumiwa kufundisha sayansi halisi." Aliituhumu elimu ya Al-Zaitouna kuwa ngumu na ya kiwango cha chini. Kusudi halisi wakati huo kwa madai ya mageuzi ya elimu ilikuwa ni kuingiza umagharibi ndani ya jamii nchini Tunisia, ikiitenganisha kwa makusudi kutokana na Dini na Ummah ili kuhakikisha mwendelezo wa thaqafa ya Kimagharibi na kuitawala kifikra jamii, na kuunda "wasomi" wa kisekula walio waaminifu kwa mkoloni Magharibi ambao watatumikia maslahi yake kwa muda mrefu na kuingiza sumu zake ndani ya akili za watu ili kuwezesha utiishaji wao wao. Hili liligunduliwa wakati Chuo Kikuu cha Al-Zaitouna, mojawapo ya vyuo vikuu vikongwe ulimwenguni, ambacho kimetoa maelfu ya wasomi tambulika, kilipofungwa. Zawatna (wahitimu wake) walihamishwa, na elimu ya kisekula ikawekwa.

Hata hivyo, mwelekeo huu wa kuingiza umagharibi ulifichua mapungufu yake, na kila mmoja alishuhudia kuanguka kwa kiwango cha elimu. Mazungumzo ya mageuzi yalitokeza tena, na mageuzi yanayodhaniwa yalikuja wakati wa miaka ya mapema ya utawala wa Ben Ali. Alijulikana kwa mradi wa "ukaushaji vyanzo" (yaani kukausha vyanzo vya Uislamu), kutekelezwa na waziri wake, Mohamed Charfi, mmoja wa wanachama wa kipote cha wasomi wa kisekula waliozaliwa na "Mageuzi ya elimu yalioingizwa Umagharibi." Mnamo 1991, baada ya miongo kadhaa ya uingizaji umagharibi na usekula, Charfi alirudi kwenye mfumo wa elimu uliopita ili kuuimarisha kwa kuondoa athari zozote zilizobakia za Uislamu, akijificha nyuma ya kauli mbiu yenye sumu "Kutoka kitambulisho cha kitaifa hadi kitambulisho cha kiulimwengu".

Kufeli kulijirudia na mporomoko ukazidi hadi elimu ilibadilika kutoka hali ya mgogoro hadi kuwa mzalishaji wa migogoro. Shule, ambapo awali ilikuwa ni nafasi ya elimu, ikawa ni nafasi ya kuharibu maadili. Mamlaka ziliachana na dori yao, kupuuza elimu kabisa. Taasisi ziliachwa kupuuzwa hadi kufikia wakati habari za dari kuangukia wanafunzi zikawa ndio tukio la kawaida. Walipuuza walimu, na kuwaacha chini ya ngazi ya ajira licha ya wao kuwa watendaji msingi katika mchakato wa elimu, walimu, iwe waelimishaji au maprofesa, walikabiliwa na udhalilishaji, mpaka hata kusubutu vitendo vya watapeli. Yote haya yalifichuliwa ndani ya sera ya makusudi kusukuma watu kwenye elimu ya kibinafsi, na kuigeuza elimu kuwa chanzo cha mapato na ufujaji kwa wakubwa waliobahatika na wenye fedha. Mamlaka ziliachana na dori yao katika kutoa huduma, na fahamu ya elimu bila malipo ikawa si chochote zaidi ya kauli mbiu tupu. Wakati wote huu watu walikuwa wakivumilia hali ya maisha isiyojali.

Wazazi wapendwa nchini Tunisia:

Hii ndio hali ya sasa ya elimu nchini Tunisia, ambayo wakoloni wa Magharibi waliitenganisha na Ummah wa Kiislamu na thaqafa yake ya Kiislamu chini ya kisingizio cha usasa na maendeleo. Hii ndio hali yetu leo baada ya mageuzi yao ya madai kwa zaidi ya nusu karne! Matokeo yake ni hali ya janga kwa vipimo vyote. Mnashuhudia kwamba watoto wenu wanaorodhesha vibaya katika tathmini za ulimwengu, na vyuo vikuu na shule zenu hazijumuishwa katika orodha za ulimwengu, na vyuo vikuu vingi katika nchi zingine za Kiafrika vikivizidi. Haifichiki tena kwenu kwamba shule mnazofadhili na bidii yenu na muhanga kila mwaka huwatupa maelfu kwa maelfu ya watoto wenu mabarabarani, katika umri ambao unahitaji msaada, utunzaji, na mwongozo. Wao hutupwa katika ukosefu wa ajira, dawa za kulevya, mashua za kifo, makundi ya uhalifu uliopangiliwa, na mafia wa vita vya kimataifa - yote kutokana na ufisadi wa elimu, katika sera, mbinu, na kusudio. Haya pia ni matokeo ya msisitizo wa watawala bandia wa kisekula juu ya utegemezi wa kitiifu kwa Magharibi na mitaala yake.

Wazazi wapendwa katika nchi ya Zaytuna:

Imeonekana wazi kwa kila mtu aliye na ufahamu kwamba taarifa juu ya mageuzi ya elimu tangu Bourguiba hadi siku ya leo sio chochote bali utekelezaji wa ajenda za kigeni za Magharibi bila kusudi jengine isipokuwa ukoloni na utawala juu ya mataifa. Inajulikana vyema kuwa kutawaliwa kifikra na kithaqafa ndio aina hatari zaidi ya ukoloni. Mkoloni anaendelea kuingilia kati katika elimu na thaqafa yetu katika aina mbali mbali. Mashauriano yaliyodaiwa yaliyoanzishwa na Rais Kais Saied hayajakengeuka kutokana na njia za mageuzi ya madai tangu Bourguiba. Miundo yake mitano haikushughulikia madhumuni ya elimu na kanuni msingi ambazo yanapaswa kuegemea juu yazo. Maswali yote yalilenga njia na mbinu katika mchakato wa elimu, kama vile kufanya chekechea na shule za Quran kuwa za lazima au la, idadi ya masaa ya shule, idhini ya vikao vya usaidizi, na upendeleo wa kuweka uzoefu wa shule za mfano na taasisi. Hata wakati ilizungumzia mhimili wa "mipango ya kufundisha, mfumo wa tathmini, na wakati wa shule," haikuingia katika yaliyomo ndani ya programu hizi na kanuni za msingi. Hii inaibua swali: ni nani anayesimamia uundaji wa maswali ya mashauriano? Je! yalibuniwa kwa msingi gani wa kifikra? Je! Yaliegemea juu ya msingi wa Uislamu? Jibu bila shaka ni hapana. Kwa hivyo, nini kitabadilika basi? Nani atasimamia utekelezaji wa matokeo ya mashauriano? Je! Sio kundi lile lile la kisekula ambalo linaitukuza Magharibi na kusimamia utekelezaji wa "mageuzi" yaliyopita? Hili linathibitisha kuwa mchakato wa mageuzi hautazidi ukarabati na kuweka mfumo wa elimu uliopita ndani ya mfumo wa kanuni ya kisekula ya kibepari ya usasa ambayo imesababisha tu utasa na kufeli nchini Tunisia.

Waislamu katika ardhi ya Zaytuna ya vyuo vikuu vya zamani vya kifahari zaidi:

Hakika, tunaelewa hamu yenu ya kushuhudia mwisho wa mifumo ya kisasa ya elimu ya kisekula iliyofeli katika nchi zetu za Kiislamu. Tunatambua hamu yenu ya muundo angavu wa kielimu. Katika Hizb ut Tahrir Wilayah Tunisia, tunawasilisha mfumo wa elimu wa hali ya juu ulioainishwa katika rasimu ya Katiba ya Dola ya Khilafah ya Hizb ut Tahrir na kitabu chake, Misingi ya Mtaala wa Elimu katika Dola ya Khilafah. Mfumo huu unashughulikia malengo na mitaala ya kielimu pamoja na njia na mikakati ya kufundishia, yote yamewekwa kwa dalili za Kisharia. Baadhi ya sifa zake muhimu ni pamoja na:

1. Ni mfumo wa kielimu ulioegemezwa juu ya ubwana ni wa Sharia na mamlaka ni ya Ummah, huru kutokana na ushawishi wa Magharibi kwenye mitaala yake au kulazimishwa kwa malengo ya kisasa ya kisekula na vipote vya wasomi yaliyotenganishwa na Ummah. Badala yake, sera na malengo ya kielimu yanaundwa kwa mujibu wa njia ambayo huhifadhi kitambulisho na imani za Kiislamu za Ummah. Hili linakusudia kuzalisha shakhsiya za Kiislamu zenye aqliya na nafsiya za Kiislamu, kuwaandaa watoto wa Waislamu kuwa wataalamu katika nyanja zote za maisha, ikiwemo sayansi ya Kiislamu (kama fiqh, theolojia, na mfumo wa mahakama) na sayansi za majaribio (hisabati, habari, kemia, fizikia, udaktari, nk).

2. Msingi wa mweleko huu wa kielimu ni Itikadi ya Kiislamu (Aqida), inayounda vifaa vya masomo pamoja na njia za kufundishia ili kuoana na msingi huu. Kuifanya itikadi ya Kiislamu kuwa ndio msingi inamaanisha kuwa maarifa yanayohusiana na imani na kanuni lazima yachipuze kutokana na itikadi ya Kiislamu. Ujuzi na kanuni zisizohusiana na imani zinajengwa juu ya itikadi ya Kiislamu, kwa kuitumia kama kipimo. Kitu chochote kinachogongana na itikadi hiyo kinakataliwa, kama vile madai kwamba wanadamu walitokana na nyani, huku maarifa yasiyogongana kama sayansi ya matibabu, mazingira, na ya kihesabu inakubaliwa.

3. Hoja ya tatu muhimu ni uwepo wa mfumo wa Khilafah, mfumo wa kisiasa wa hali ya juu. Mfumo wa Khilafah una ruwaza ya wazi na uhuru ya kisiasa, ukizingatia elimu kama kiwanda cha kuzalisha viongozi wa hali ya juu. Inapanda msingi wenye rutuba wa kukuuza shakhsiya imara zinazotamani uongozi, zikikataa unyenyekevu wa kudhoofisha. Dola ya Khilafah inaweka kipaumbele sekta ya elimu kwa sababu ya dori muhimu ya elimu, iliyoambatana na mtazamo wa Uislamu kwamba elimu na imani ni mapacha. Dola hutoa elimu bila malipo kwa kiwango cha juu kabisa, pamoja na huduma ya afya na usalama, kuhakikisha mahitaji msingi yanafikiwa kwa kila mtu binafsi.

Dola ya Khilafah itarekebisha vipaumbele vyake kulingana na hukmu za Sharia, kuongeza kasi ya maendeleo ya kisayansi. Itatenga mapato muhimu kutoka kwa mali ya umma, ikiwemo madini, kawi, kilimo, na utajiri wa wanyama, ili kujenga mifumo midogo inayosaidia uwezo wake katika kufikia viwango vya juu vya elimu. Hii ni pamoja na:

Kwanza: Kuunda mfumo mpana wa elimu kuanzia wa kiwango cha msingi hadi sekondari na kiwango cha juu, kuimarisha shakhsiya za Kiislamu kuwa viongozi wanaolinda maswala muhimu ya Ummah na uwezo wa kuunda mikakati. Kwa hivyo, kizazi kitaundwa ambacho kinachanganya sifa za uongozi na uaminifu wa muumini, na chenye kufurahiya ujuzi mbali mbali na maeneo ya uzoefu ambayo Ummah anahitaji katika nyanja za maisha.         

Pili: Kuanzisha mfumo wa utafiti na maendeleo, kuoanisha vyuo vikuu na vituo vya utafiti vinavyomilikiwa na serikali chini ya usimamizi, ushajiishaji, na ufadhili wa serikali.

Tatu: Kuunda mfumo huru wa kimkakati wa viwandani, kuusimamia kwa uhuru. Hii itaimarisha uwezo wa kijeshi pamoja na mbinu za kisasa, kutoa mahitaji msingi kwa watu binafsi. Itaunda silsila oanishi za viwanda vizito chini ya usimamizi wa serikali, kupata usambazaji wote muhimu, ikiwemo malighafi, teknolojia, utaalamu, uhandisi, na ufadhili.

Waislamu, mfumo wa Khilafah, kutabanni mtazamo tofauti wa Kiislamu juu ya elimu, yana uwezo leo wa kuanzisha mfumo wa kipekee wa elimu. Unachanganya utafutaji elimu na utimizaji wa maswala nyeti na maslahi ya dola pamoja na umma. Wakati huo huo, inahakikisha kujitosheleza katika mahitaji yote ya umma, kuondoa utenganishaji kati ya mifumo yetu ya kielimu na mahitaji ya jamii zetu za viwandani, kilimo, na teknolojia, kuzuia utegemezi wa nchi zengine. Hii, ni pamoja na uwekezaji mkubwa katika utengenezaji, itakidhi mahitaji ya jamii kwa kujitegemea, ikiiweka Khilafah kama dola ya kiulimwengu. Inawezesha dola kunufaika na ujuzi na akili za kipekee za Ummah kwa maendeleo ya dola, kuhakikisha uwezo wao wa thamani haupotei au kunyonywa na nchi za kigeni.

Waislamu, harakisheni kutabikisha na kutekeleza muundo huu bora mara moja. Timizeni kazi muliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu ya kusimamisha Khilafah Rashida, kwani ndio suluhisho pekee la halali kwa maswala yenu yote. Kama Mwenyezi Mungu (swt) anavyosema:

[الَّذِينَ إِن مَّكَّنَّاهُمْ فِي الْأَرْضِ أَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ وَأَمَرُوا بِالْمَعْرُوفِ وَنَهَوْا عَنِ الْمُنكَرِ وَلِلَّهِ عَاقِبَةُ الْأُمُورِ]

“Wale ambao tukiwapa madaraka katika nchi husimamisha Sala, na wakatoa Zaka, na wakaamrisha mema, na wakakataza mabaya. Na kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo ya mambo yote.” [Surat Al-Hajj:41].

H. 18 Jumada I 1445
M. : Jumamosi, 02 Disemba 2023

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Tunisia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu