Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Serikali ya Kihalifu jijini Damascus Inaporomoka na Inahitaji Juhudi ya Dhati Kuipindua
(Imetafsiriwa)

Haifichiki tena machoni mwa waangalizi kwamba hali katika maeneo yaliyo chini ya usimamizi wa serikali ya kihalifu jijini Damascus imefikia kiwango kisichoweza kuvumilika. Mambo msingi ya maisha yamepotea, na kutoa njia kwa umaskini, njaa, na kutawala kwa wanamgambo wa mauaji, uporaji, na uhalifu, pamoja na vifaa vya ukandamizaji na mauaji. Hii imelazimisha watu katika maeneo mbali mbali kuchukua hatua kwa mara nyengine tena, kuchochea upya moto wa mapinduzi ambayo yangali yanawaka ndani ya nyoyo za watu wa Ash-Sham. Wanarudisha tena harakati za mapinduzi ambapo miito ya Mapinduzi inasikika, wito mkuu ukiwa kupinduliwa kwa serikali ya jinai.

Maandamano hayo yameregeshwa tena katika miji mingi, pamoja na Daraa, kitovu cha Mapinduzi, na kwengineko. Miito ya mapinduzi yenye baraka ya Ash-Sham, "Kifo badala ya udhalilifu" na "watu wanataka kuiangusha serikali" imesikika kwa mara nyingine tena. Hii inafuatia harakati iliyobarikiwa ambayo ilianza katika maeneo ya kaskazini yaliyokombolewa dhidi ya madhalimu wote na wakuu waliokiuka matukufu, wakawakandamiza watu, na kula njama dhidi ya mapinduzi ya Ash-Sham na watu wake.

Kama kawaida kwa madhalimu, iwe ni wa kiwango cha juu au kiwango cha chini, na kama kawaida kwa nchi zinazokula njama dhidi ya mapinduzi ya Ash-Sham, majaribio yameanza kupotosha mwendo wa harakati mpya za mapinduzi mbali na mipaka ya mapinduzi ya Ash-Sham. Hili linafanywa kwa kupotosha matakwa yake, kuyafunga katika upataji riziki na mambo yanayohusiana na huduma wakati mwingine, na kuyaelekeza kwa kiasi kwenye miradi ya mgawanyiko wakati mwingine. Kwa kuongezea, kuna jaribio la kudhibiti harakati ya umma na kuionyesha kama matakwa ya suluhisho la kisiasa la Marekani, na kutekeleza azimio 2254, ambalo huhifadhi serikali ya mauaji na uhalifu na katiba yake ya kisekula, hata kama nyuso za watendaji na washirika zitabadilika.

Katika kutafuta hili, wamemuangazia kwenye vyombo vya habari mtu yeyote aliye tayari kutumikia miradi yao na suluhisho lao hatari la kisiasa. Wamewawasilisha kama viongozi wa harakati mpya za mapinduzi, huku wakificha na kupotosha harakati za kweli za wenye ikhlasi. Hili ni jaribio la kuchukua uongozi wa harakati ya umma na kuipotosha kutoka kwa njia yake iliyokusudiwa.

Kwa kukabiliwa na mpango huu wa kijanja, Mapinduzi ya Ash-Sham na harakati zake mpya lazima zishikamane na mipaka ya mapinduzi yenye baraka ya Ash-Sham ili kukwepa njama zilizoandaliwa dhidi yake. Ni muhimu kwa Mapinduzi ya Ash-Sham yenye baraka kufuata kanuni hizi za msingi:

1- Kuendeleza mapinduzi hadi serikali ya jinai itakapopinduliwa na utawala wa Uislamu kusimamishwa mahali pake, bila kutilia maanani mabadiliko ya hadaifu ya kulemaza.

2- Kukomesha uingilia kati wa nchi za ulaji njama katika mapinduzi ya Ash-Sham na kukata mafungamano nazo, kukataa aina zote za msaada kutoka kwao. Tumeshuhudia jinsi msaada wa nchi hizi na sera zao za njama umetusababisha hasara, na kutelekezwa, wakati mapinduzi yalikuwa karibu na kuipindua serikali ya jinai ambayo ilikuwa imekwamia jijini Damascus.

3- Simamisheni uongozi wa kisiasa wa dhati na wenye ufahamu miongoni kwa ndugu na watoto wetu, watu ambao wamethibitisha uaminifu wao, uthabiti, ujasiri, na uhuru kupitia misimamo na majaribio yao. Kataeni uongozi wote wa kutengenezwa unaohusishwa na miradi ya kimataifa na ajenda za nje za njama. Wakataeni wale ambao wamekumbatia kamba za walaji njama, wakawakandamiza watu wa mapinduzi ya Ash-Sham, na wakadandia mihanga yao.

4- Kuungana pambizoni mwa mradi wa wazi wenye kuunganisha uliochipuka kutoka katika Aqida yetu, tunashikamana imara na kamba ya Mwenyezi Mungu na kukata mafungamano na wengine wote. Tunaweka imani yetu tu kwa Mwenyezi Mungu, tukimtegemea kwa usalama na msaada, kwani ushindi uko tu mikononi mwake pekee, Azza wa Jal. Huwaruzuku kwayo wakweli miongoni mwa waja wake. Hakika, ametuarifu kupitia maneno yake:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Muhammad: 7]

Enyi Wanamapinduzi wa kweli katika Ardhi ya Ash-Sham:

Miaka ya Mapinduzi ya muda mrefu imethibitisha kuwa mapinduzi ya Ash-Sham ni thabiti dhidi ya njama zote, haijalishi ni kubwa kiasi gani. Moto wa mapinduzi ungali unawaka ndani ya nyoyo za watoto wake. Ikiwa tunashikilia kanuni zetu na kubaki wakweli kwa Mwenyezi Mungu katika misimamo yetu, kamwe hatatuacha. Nusra yake itakuwa pamoja nasi, na ushindi wake utakuwa wetu, Inshallah.

Basi hebu na tusonge mbele kwa maono, tukiweka imani yetu tu kwa Mwenyezi Mungu, hadi tuipindue serikali ya kihalifu pamoja na katiba yake, vyombo vyake vyote, na nembo, ili kusimamisha utawala wa Uislamu chini ya kivuli cha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Khilafah hii itaokoa waumini na kuwaletea furaha katika ulimwengu huu na Akhera, ikimridhisha Bwana wa viumbe vyote. Anasema katika wahyi wake ulio wazi:

[إِن يَنْصُرْكُمُ اللهُ فَلَا غَالِبَ لَكُمْ وَإِن يَخْذُلْكُمْ فَمَن ذَا الَّذِي يَنصُرُكُم مِّنْ بَعْدِهِ وَعَلَى اللهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ]

“Akikunusuruni Mwenyezi Mungu hapana wa kukushindeni, na akikutupeni ni nani, basi, baada yake Yeye ataye kunusuruni? Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu.” [Aali-Imran: 160].

H. 9 Safar 1445
M. : Ijumaa, 25 Agosti 2023

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Syria

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu