Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mamlaka ya Palestina Yadhihirisha Ukweli wa Msimamo Wake Kupitia Kukishambulia Kisimamo Kinacho Kataa Mkataba wa Trump

[وَإِنَّ الظَّالِمِينَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ وَاللَّهُ وَلِيُّ الْمُتَّقِينَ]
“Na hakika wenye kudhulumu ni marafiki wao kwa wao. Na Mwenyezi Mungu ni rafiki wa wamchao.” [Al-Jathiya: 19]

 (Imetafsiriwa)

Mnamo Jumamosi asubuhi, 15 Februari 2020, Mamlaka ya Palestina (PA) na vyombo vyake vya usalama iliweka vizuizi katika lango la kuingilia mji wa Jenin, na kuchukua hatua kadhaa ili kuzuia kisimamo kilichoitishwa na Hizb ut Tahrir ili kupinga mkataba wa kikoloni wa Trump, … na punde tu baada ya kisimamo hicho kuanza watu wake walijitokeza katika hali ya jazba na uadui kuwakandamiza watu katika mandhari ya aibu ikidhihirisha ukweli wa vyombo hivi  vilivyoletwa na Jenerali Dayton wa Marekani, na watu kupaza sauti za Allahu Akbar (Mwenyezi Mungu ni mkubwa), na kutangaza ukweli wakitafuta ushindi wa Ummah wa Kiislamu na majeshi yake ili kuikomboa Ardhi Tukufu na sauti ya ukweli ikiibua kukataa kujisalimisha na suluhisho la khiyana. Hivyo basi, ni nini kilicho ikasirisha PA na vyombo vyake hadi kuwashambulia watu kwa njia ya kinyama, ikifyatua mabomu ya gesi na risasi, na kulipiga bango la Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) “La Ilaha illa Allah, Muhammad Rasul Allah”, kwa magongo na kuwashambulia wazee na Sheikh mkubwa mwenye umri wa miaka tisini?! 

Tunamuuliza gavana wa Jenin, Akram al-Rajoub, mkurugenzi wa ujasusi, Muhammad Ghannam, na mkurugenzi wa ulinzi, Hijazi al-Jabari, ni kipi kilicho wakasirisheni katika kisimamo hiki? Je, mulikasirishwa na idadi kubwa ya takbir za watu (wakisema Allahu Akbar) … au ni bango la Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)?! Au na mwito kwa Ummah wa Kiislamu na majeshi yake kuikomboa Ardhi hii Tukufu, au kwa kukataa suluhisho la khiyana lililoipa umbile la Kiyahudi asilimia 78 ya Ardhi hii Tukufu?! … Semeni kile kilicho wakasirisheni?! Je, Sheikh Taher, ambaye ana takriban umri wa miaka tisini, aliyesimama mbele yenu madhalimu, akipaza sauti ya Allahu Akbar na kuwashajiisha Waislamu, ndiye aliye wakasirisheni?! Tunaapa kwa Mwenyezi Mungu, ambaye hakuna mungu isipokuwa Yeye, kheri hii haiwakasirishi isipokuwa Mayahudi na maadui wa Uislamu … Hivyo basi, je, nyinyi muko upande wao?! … Jibuni: Je, nyinyi muko upande wa Mayahudi na maadui wa Uislamu?!

Enyi Watu ndani ya Ardhi Tukufu:

Ukweli wa Mamlaka ya Palestina (PA) na jukumu lake msingi lilidhihirishwa waziwazi na Rais wa PA katika kongamano la mwisho la Kiarabu, na aliliambia umbile la Kiyahudi, “Sasa nina uwezo wa kulinda … Nina uwezo wa kukuleteeni kipande cha taarifa ambayo kamwe hamujawahi kuiota”. Akaongeza, “Tuna mikataba na makubaliano 83 na tuko tayari kushirikiana na nchi yoyote inayopigana na ugaidi na tunafuata sera hii na kamwe hatutarudi nyuma kutokana nayo!” Na akasisitiza hili katika hotuba yake katika Baraza la Usalama na akaongezea kuwa yuko tayari kutoa huduma mpya za usalama zitakazo panuka hadi nchi 183 … Hivyo, huu ndio ukweli wa PA, si lolote isipokuwa ni mkono tu wa usalama unaotumikia maadui wa Uislamu. 

PA na vyombo vyake ni warongo katika kukataa mkataba wa Trump, hivyo yeyote anaye isalimisha asilimia 78 ya ardhi ya Israa na Mi'raj katika Mkataba wa Oslo hakumdhuru kusalimisha asilimia 82 katika mkataba wa Trump, lakini khiyana inayohitajika kutekeleza mkataba huu ni kubwa zaidi kuliko PA, na Marekani na Mayahudi wanacheza kamari katika kuyatayarisha mazingira kwa ajili ya utekelezaji wa miradi yao ya kikoloni. Kwani umbile la Kiyahudi limewekeza katika makubaliano ya Oslo kama pazia ili kuunda uhalisia mpya katika Ukingo wa Magharibi, na walishacheza kamari juu ya PLO iliyo telekeza mkataba wake na kukubali kulitambua umbile la Kiyahudi na kuisalimisha takribani Palestina yote baada ya kusema la tatu; la kwa utambuzi wa umbile la Kiyahudi, la kwa amani, na la kwa majadiliano pamoja na adui wa Kizayuni.  

Kukataa kwa PA mkataba wa Trump ni ukataaji tu wa kisanii na sio wa kiuhakika. Mikataba ya "Beilin-Abbas" na "Olmert-Abbas" haina tofauti sana na mkataba wa Trump isipokuwa katika baadhi ya maelezo. Kinacho thibitisha kuwa upinzani wa mamlaka hayo ni wa kisanii na sio wa kiuhakika ni kutangaza kwake kujitolea katika vita dhidi ya ugaidi "yaani vita dhidi ya Uislamu" na utiifu wake kwa maazimio na makubaliano ya kimataifa iliyo yatia saini pamoja na umbile la Kiyahudi, ambayo kwayo iliisalimisha takribani Palestina yote, kujitolea kwake kwa mradi wa khiyana wa Kiarabu na kujitolea kwake kwa chaguo la majadiliano, kama inavyo jitolea kwa kila kitu kinacho hifadhi umbile la Kiyahudi na kulipa uhalali kati Ardhi Tukufu ya Palestina. Hivyo basi umbile la Kiyahudi litabakia na hakikisho kuwa utekelezaji wa miradi yake utabakia maadamu Mamlaka hayo yatajitolea katika dori yake ya usalama na yanatoa mwito kwa jamii ya kimataifa, Baraza la Usalama na Umoja wa Mataifa, kwa sababu mwito huu ni sawa na kilio ndani ya bonde ambacho hakimpi afueni wala kumuokoa mtu.   

Uhalifu uliofanywa na PA dhidi yenu na kadhia yenu kamwe haujakoma, kama ambavyo haujakoma uhalifu wa kuisalimisha ardhi yenu kwa adui yenu, bali iliwafanya watu kuonja moto wa usimamizi wake "mtukufu" wa usalama kwa uvamizi huo, na haikuacha mlango wowote wa kuwafisidi watoto wetu na kuyaharibu maadili ya Uislamu ndani ya nafsi zao isipokuwa iliufungua, na mumeona kudumu kwake kubadilisha sheria ya hadhi ya kibinafsi ili kuafikiana na makubaliano ya kihalifu ya CEDAW, na kuwasheheni watu kwa mikopo na madeni kutokana na sera yake ya kiuchumu ya kuwafanya watu wafungike na mikopo ya nyumba ya mabenki … Na ufisadi kutawala ndani ya taasisi zake hadi PA ikawa ndicho kitovu cha ufisadi … Haitarajiwi kukomesha uhalifu wake, kwani nyoyo za viongozi wake zimezama katika kuwategemea maadui wa Uislamu.   

Enyi watu ndani ya Ardhi Tukufu:

Yale ambayo maadui zenu wanapanga dhidi yenu ni makubwa, na yale muliyo pangiwa ni uhalifu mkubwa zaidi kuliko yale yaliyotokea mwaka wa 48 na 67, hivyo umbile la Kiyahudi linatafuta kuifanya Palestina kuwa ardhi yake pekee, na uhalifu huu kamwe hauwezi kukomeshwa kupitia Baraza la Usalama na Umoja wa Mataifa wala Quartet (muungano wa nchi na jumuia nne za kimataifa ambazo ni Umoja wa Mataifa, Marekani, Muungano wa Ulaya na Urusi zinazo simamia mapatano ya amani kati ya "Israel" na Palestina) … nk. وَالَّذِينَ كَفَرُوا بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ "Na wale walio kufuru ni marafiki wenyewe kwa wenyewe." [Al-Anfaal: 73].

Mumepitia maazimio ya kimataifa; lengo lake ni kuwapurukusha na kuwanyamazisha watu! Kisha yale tu yaliyo na maslahi kwa maadui wa Uislamu pekee ndiyo yatakayo tekelezwa … Ama kuhusu misimamo ya viongozi wa mamlaka hayo na watawala wa ulimwengu wa Kiislamu, ni ya fedheha na uzembe, kwa sababu wamekhini kadhia yenu kwa muda mrefu, hivyo musisubiri kheri kutoka kwao.

Suluhisho la kimsingi la kadhia ya Palestina ni kuirudisha katika asili yake; katika upeo wake halisi, nao ni Uislamu na Ummah wa Kiislamu, kwani hii ndio njia sahihi na halali kwa fahari yenu, na ndiyo ambayo maadui zenu wanafanya kazi mchana na usiku kuwaweka mbali nayo. Kinachotia hofu ndani ya nyoyo za maadui zenu ni kuwalingania Ummah na majeshi yake kutoa msaada ili kusimamisha Khilafah, na Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu ili kuitakasa Ardhi hii Tukufu kutokana na najisi ya wanyakuzi … Marekani na Mayahudi wanatishiwa na Uislamu na kurudi kwa Khilafah, na ukweli wa Mayahudi na uadui wao kwetu sisi na Uislamu uko wazi katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu anayesema:  

 [لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ النَّاسِ عَدَاوَةً لِلَّذِينَ آمَنُوا الْيَهُودَ وَالَّذِينَ أَشْرَكُوا]

“Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walio amini ni Mayahudi na washirikina.” [Al-Ma’ida: 82].

Naye Yeye (swt) asema:

[أَمْ لَهُمْ نَصِيبٌ مِنَ الْمُلْكِ فَإِذاً لَا يُؤْتُونَ النَّاسَ نَقِيراً]

“Au wanayo sehemu ya utawala? Basi hapo wasingewapa watu hata tundu ya kokwa ya tende.” [An-Nisa: 53[.

Na Mwenyezi Mungu ametuhakikishia kuidhihirisha dini Yake, na Mtume wake (saw) ametupa bishara njema ya Khilafah kwa njia ya Utume na Mwenyezi Mungu kamwe havunji ahadi Yake, hivyo basi muaminini Mwenyezi Mungu mlinzi wenu na msaidizi wenu … Uaminini Ummah wenu, uliobora zaidi uliotolewa kwa watu, na shikamaneni na maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اصْبِرُوا وَصَابِرُوا وَرَابِطُوا وَاتَّقُوا اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ]

“Enyi mlio amini! Subirini, na shindaneni kusubiri, na kuweni macho, na mcheni Mwenyezi Mungu, ili mpate kufanikiwa.” [Al-i-Imran: 200]

  [وَاعْتَصِمُوا بِاللَّهِ هُوَ مَوْلَاكُمْ فَنِعْمَ الْمَوْلَى وَنِعْمَ النَّصِيرُ]

“na shikamaneni na Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mlinzi wenu, Mlinzi bora kabisa, na Msaidizi bora kabisa.” [Al-Hajj: 78[.

Shikamaneni na maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا لَقِيتُمْ فِئَةً فَاثْبُتُوا وَاذْكُرُوا اللَّهَ كَثِيراً لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ * وَأَطِيعُوا اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَلَا تَنَازَعُوا فَتَفْشَلُوا وَتَذْهَبَ رِيحُكُمْ وَاصْبِرُوا إِنَّ اللَّهَ مَعَ الصَّابِرِينَ]

“Enyi mlio amini! Mkikutana na jeshi, basi kueni imara, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu sana ili mpate kufanikiwa. * Na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu. Na subirini. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao subiri.” [Al-Anfal: 45-46[.

H. 23 Jumada II 1441
M. : Jumatatu, 17 Februari 2020

Hizb-ut-Tahrir
Ardhi ya Baraka-Palestina

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu