Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Usaliti na Ufisadi wa Mamlaka ya Palestina ni Jinai Kubwa Dhidi ya Palestina na Watu wa Palestina!
(Imetafsiriwa)

Abbas bwege na genge lake, ambao wamemsaliti Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake, tangu kutiwa saini kwa Mkataba wa khiyana wa Oslo, na wamekuwa wakifanya kazi kwa utaratibu na uratibu pamoja na umbile la Kiyahudi, ili kuimaliza ari ya jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) miongoni mwa watu wa Palestina ili kukomesha “mateso ya Mayahudi,” wanashirikiana dori kwa njia ovu. Wale ambao Mwenyezi Mungu (swt) amewakasirikia wanatuua na kutuangamiza. Uhalifu wao haukomi; kuanzia kuwaua Mujahidina, wanawake na watoto, kubomolewa nyumba na kunyang’anya ardhi mpaka makaazi yakawa ni tezi ya saratani inayotafuna vilivyoko pambizoni mwake, na makundi ya walowezi yanazunguka kwenye milima na barabara kwa kuwafanyia uadui watu na Mamlaka ya khiyana na huduma zake za usalama huwafuatilia watu, kufanya uratibu na uvamizi huo na kuupatia taarifa. Hata hivyo, hili sio hatari zaidi kuliko uhalifu wake.

Umbile la Kiyahudi na nchi za Magharibi zilitambua kwamba haziwezi kubaki katika ardhi hii isipokuwa kwa kuwatenganisha watu wa Palestina na Dini yao, kubatilisha kitambulisho chao na kusambaratisha familia zao. Hili linaweza tu kupatikana kupitia kuwalenga wanawake, familia na watoto, ili kuunda vizazi vipya, "Mpalestina mpya" anayehubiriwa na Jenerali wa Marekani Dayton. Sawa na huduma za usalama, ambazo aliziita "Mpalestina mpya" ambaye anasimama bega kwa bega na jeshi linaloikalia kwa mabavu.

Mamlaka ya Palestina imefungua mlango mkubwa kwa taasisi zinazofadhiliwa na nchi za Magharibi kueneza sumu yao na kutekeleza mipango yao ya kifisadi, na inafanya kazi kwa bidii kufadhili kile kinachofisidi maadili na kuangamiza mujtamaa katika nyanja zote, na inafanya kazi kwa bidii kutafuta mfumo wa sheria unaofadhili na kulinda ufisadi huu. Chini ya jina la "uamuzi wa sheria" matukufu yamekiukwa, kwani Mamlaka ya Palestina hivi leo inafanya kazi kwa bidii kurekebisha sheria ili kuimarisha malengo ya maadui wetu na umbile la Kiyahudi, ikiwemo sheria zinazolenga familia zetu, watoto, na mtaala wetu. Hili linaambatanishwa na sera ovu ya vyombo vya habari ambayo hutoa ufadhili na propaganda kwa shughuli za ufisadi, pamoja na sera ya kiuchumi inayolenga kupanua ukusanyaji ushuru na kuongeza ushuru. Kulinda ukiritimba kwa ajili ya kipote cha wanyonyaji damu, kuwatupa watu kwenye madeni na kuweka rehani mali zao kwa mabenki.

Enyi watu wa Ardhi Iliyobarikiwa: Juhudi za Mamlaka ya Palestina kutekeleza sera za umbile la Kiyahudi na nchi za Magharibi ambazo zinalenga kuangamiza familia zetu, kuwazika mabinti zetu wakiwa hai na kuwaua watoto wetu kwa kuwavua Dini yao, chimbuko la fahari na amani yao na njia ya kukomboa ardhi yao, yote haya ni jinai kubwa dhidi ya Palestina na watu wa Palestina, ambayo ina maanisha kwamba mamlaka na wale walio nyuma yake wanafanya kazi, kuwanyang'anya watoto wetu kutoka kwa familia zetu ili watoto wetu wasiwe na kitambulisho au lengo na wafanye kazi ili kuutumikia uvamizi huo, kama vile huduma za usalama.

Enyi Watu Wetu na Wapendwa wetu: Kanuni za utendaji za Sheria ya Ulinzi wa Mtoto iliyochapishwa katika Gazeti la Al-Waqa'i mnamo tarehe 25/9/2022 ni utabikishaji wa Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto, ambao umeegemezwa juu ya fahamu potovu za Kimagharibi, na tunakuonyeni vikali dhidi yake.

Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto ulifanywa ndio maregeo katika utangulizi wa azimio hilo, na wakati wa kufafanua maslahi bora ya mtoto, uliufanya Mkataba huo kuwa ndio maregeo yake. Unabainisha (kuhakikisha mtoto anafurahia kikamilifu na vyema haki zote zinazotambuliwa katika mikataba na sheria husika ya kimataifa...), maslahi ya mtoto yanaamuliwa kulingana na mikataba ya kimataifa na fahamu za Kimagharibi, sio Uislamu. Kisha kifungu cha pili, Ibara ya 4, kilisema (Kumlinda mtoto dhidi ya aina zote za ubaguzi kwa misingi ya jinsia, dini, lugha au maoni ya kisiasa) na maana ya aya hii iko wazi. Jinsia ya mtoto ni ya kiume au ya kike, na jinsia yake ya kijamii ni hisia ya mtoto kwamba yeye ni mwanamume au mwanamke, bila kujali jinsia yake, na hii inajumuisha sheria ya kuhalalisha na kulinda ushoga. Hii ina andamana na kile ambacho Mkataba wa Haki za Mtoto unahakikisha uhuru wa mtoto kuchagua dini na imani yake. Kwa mujibu wa sheria hii, amri ya baba kwa binti yake kuvaa mavazi ya Kiislamu imekuwa ni uhalifu wa ubaguzi, kuwazuia watoto wake kutokana na ushoga ni uhalifu wa ubaguzi, na kuwazuia kutokana kuritadi Uislamu ni uhalifu wa ubaguzi. Matumizi ya sheria hii ni mapana, na inalenga kuwafanya watoto wetu waasi Dini yao, Ummah wao na baba zao.

Mamlaka ya Palestina, taasisi, jumuiya na vyombo vya habari vinawavamia watoto wetu kwa fahamu na maadili ya Kimagharibi asubuhi na jioni, na sheria hii imekuja kuwalinda na kuwazuia wazazi au watu wengine kuwafunga watoto wetu kwa fahamu za Uislamu. Ushahidi bora ni kuharamisha adhabu ya kimaneno au ya kimwili kama aina ya unyanyasaji. Hivyo wazazi watapoteza uwezo wa kuwazuia watoto wao na maovu na maadili mabaya, na tuliona matumizi ya sheria hii mashuleni hadi yakamfanya mwalimu apoteze ubora wa kielimu na uwezo wake wa kuwadhibiti wanafunzi na kuwaelekeza tabia zao, jambo ambalo liliwafanya baadhi ya wa wanafunzi kuwatukana dhahiri walimu wao, na kwa mujibu wa sheria hii, Hadith hii ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ikawa ni hatia:

«مُرُوا أَبنَاءَكُمْ بِالصَّلَاةِ لِسَبْعِ سِنِينَ، وَاضْرِبُوهُمْ عَلَيهَا لِعَشْرِ سِنِينَ، وَفرِّقُوا بينهُمْ فِي الْمَضَاجِعِ»

“Waamrisheni watoto wenu kuswali wakiwa na umri wa miaka saba, na wapigeni kwa (kutoswali) wakiwa na miaka kumi, na watenganisheni (wavulana na wasichana) katika malazi.” (Imepokewa na Ahmad kwa Isnad Sahih).

Mtoto, kulingana na ufafanuzi na madai yao, ni mtu chini ya umri wa miaka kumi na nane, na hii ni kuua shakhsiya za watoto wetu. Miongoni mwa watoto wa Ummah ni wale waliopata ushujaa na ushindi wakiwa chini ya umri huu. Kwa mujibu wa vikwazo vilivyowekwa na sheria hii, kulea watoto wetu kwa ajili ya kupambana, kujitahidi na kupigana jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) ni jambo lisilowezekana.

Enyi Watu na Wapenzi wetu (kwa ajili ya Mwenyezi Mungu): Jinai ambazo Mamlaka ya Palestina inazifanya dhidi ya njia yetu, wanawake wetu, watoto wetu na wapiganaji wetu ni hatari sana. Ni utekelezaji wa kivitendo wa sera za uvamizi na nchi za Magharibi na wamefanya kile ambacho uvamizi haukuweza kukifanya katika miaka iliyopita, na ikiwa tutapoteza familia na watoto wetu, ni nini kitakachobakia kwetu?

Kinachofanywa na mamlaka na baadhi ya taasisi za wanawake kwa kupatiliza kutumia baadhi ya mienendo isiyo ya kawaida au uhalifu wa mtu binafsi ili kuendeleza sheria hizi ni aina ya udanganyifu, kwa sababu sababu ya uhalifu huo ni kukosekana kwa Uislamu na kuenea kwa ufisadi unaofadhiliwa na Mamlaka na taasisi hizo zinazofadhiliwa na maadui wa Uislamu.

Na msimamo wenu mbele ya ufisadi huu na ufisadi unaofanywa na Mamlaka ya Palestina na walio nyuma yake, pamoja na kuitikia amri ya Mwenyezi Mungu ya kuilinda nafsi na familia kutokana na Moto:

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَاراً وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ)  

Enyi mlio amini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanausimamia Malaika wakali, wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayo waamrisha, na wanatenda wanayo amrishwa. [At-Tahrim: 6].

Vile vile ni Ribat (kulinda) eneo lisilo na ulinzi, Ardhi Iliyobarikiwa, na ulinzi kwa kizazi kinachounda pamoja na imani yake na uthabiti wa jihad, na kushikamana na Dini yake, ni nguvu thabiti inayosimama mbele ya umbile la Kiyahudi. Pia ni Ribat (kulinda) juu ya mpaka wa vita dhidi ya Uislamu kwa jumla, ni vita hivyo ambavyo kwavyo mwisho wa batili unakaribia, Mwenyezi Mungu akipenda.

(وَقُلْ جَاءَ الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقاً)

Na sema: Kweli imefika, na uwongo umetoweka. Hakika uwongo lazima utoweke! [Al-Isra: 81]

Harakati hii ya kishindo ya Magharibi na zana zake na wafuasi wake ya kuingiza ufisadi na kulazimisha sheria za ufisadi, ni kwa sababu ya kile wanachohisi juu ya hatari inayokaribia kwa ushawishi na hadhara yake, na kwa uundaji wake, umbile la Kiyahudi, na hatari ya kutokea msukumo wa Waislamu kuelekea kwenye mabadiliko ambayo yatafikia kilele, kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu (swt), kwa Khilafah Rashida, yenye kuheshimika, yenye nguvu na fahari inayosimamisha Dini, na kung'oa fikra na sheria za Magharibi, na ushawishi wake na vibaraka wake, kama itakavyoling'oa umbile la Kiyahudi kutoka kwenye mizizi yake.

(وَيقُولُونَ مَتَى هُوَ قُلْ عَسَى أَن يَكُونَ قَرِيباً)

na watasema: Lini hayo? Sema: A'saa yakawa karibu! [Al-Isra: 51]

H. 6 Rabi' I 1444
M. : Jumapili, 02 Oktoba 2022

Hizb-ut-Tahrir
Ardhi ya Baraka-Palestina

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu