Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Enyi Waislamu: Mnaona Jinai za Mayahudi kwenye Kivuko cha Rafah, Gaza na kwa hakika Palestina yote.

Na Watawala Hawapeleki Jeshi kwa ajili ya Kunusuru; Badala yake Wanapuuza Mistari yao Mekundu! Wameridhika na Upatanishi wa Marekani na Wafuasi wake!
(Imetafsiriwa)

Enyi Waislamu: Inatosha sasa. Ukatili unaofanywa na Mayahudi kwa watu, miti na mawe hauhesabiki! Sasa wanavamia kivuko cha Rafah, ambacho utawala wa Misri ulikichulia kuwa mstari mwekundu ambao haungekaa kimya kuhusu uvamizi dhidi yake. Lakini wekundu iligeuka kijani baada ya Mayahudi kuikalia kimabavu na utawala wa Misri kuridhika na maandamano pekee!! (Al Jazeera Breaking News,12/5/2024 - Associated Press, ikimnukuu afisa mmoja mkuu wa Misri: Misri iliwasilisha kulaani Tel Aviv, Washington, na serikali za Ulaya kuhusu shambulizi la Rafah). Al-Arabiya Al-Hadath ilikuwa imechapisha mnamo tarehe 7 Mei 2024: (Meja Jenerali Ali Hefzy, Waziri Msaidizi wa Vikosi vya Ulinzi vya zamani vya Misri, katika taarifa za kipekee kwa Al-Arabiya.net na Al-Hadath.net, zilisema kuwa mhimili wa Philadelphia ni eneo la usalama la Palestina kati ya Misri na Ukanda wa Gaza, na kusisitiza kwamba vikosi vya silaha vinalinda mipaka ya Misri kwa usalama mkubwa, na hakuna vikosi vya "Israel" vinavyoweza kukaribia kwa sababu ni mstari mwekundu. Jeshi la "Israel" limetangaza, leo, Jumanne, kwamba limechukua udhibiti kamili wa upande wa Palestina wa kivuko cha ardhi cha Rafah kinachotenganisha Ukanda wa Gaza na eneo la Misri, katika operesheni ya kijeshi ambayo ilianza jana. Magari ya kijeshi ya "Israel" yaliingia katika mhimili wa Philadelphia kwa mara ya kwanza tangu 2005, pia, moshi mkubwa uliongezeka katika eneo karibu na kivuko cha Rafah kati ya Ukanda wa Gaza na Misri huku "Israel" ikizidisha kampeni zake za kushambulia kwa mizinga, leo, Jumanne).

Enyi Waislamu:

Inasikitisha kwamba Magharibi, hususan Marekani, zinaongoza watawala katika nchi za Waislamu na kuelekeza nguvu zake katika nchi zinazolizunguka umbile la Kiyahudi, kwani haitaki majeshi yao yaingilie kati. Inatangaza hili kwa kusema: "Msipanue vita"! Inafahamu udhaifu wa umbile hili, kwani uvamizi wake umepita takribani miezi minane bila kufikia malengo yake, japo kinacholikabili ni kundi la waumini ambao ni wachache kwa idadi na vifaa. Kwa hivyo, vipi ikiwa majeshi ya Waislamu yangeingilia kati, au wale tu walio karibu na Palestina? Hili ndilo linaloisumbua Marekani... Hivyo basi, maafisa wake wanazunguka katika eneo hili kuzuia majeshi ya Waislamu kuwanusuru wananchi wa Palestina kwa kuwatia shinikizo watawala wa majeshi hayo, au hata bila ya kuwatia shinikizo! Maana wametelekeza ukombozi wa Palestina kutoka kwa uvamizi wa Kiyahudi tangu 1948 na sio kuanzia leo tu!! Yeyote anayechunguza ziara za maafisa wa Magharibi, haswa Wamarekani, ataona kuwa kwa lengo hili. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Blinken huwa hatoki kabisa katika eneo hilo. Marekani haikuridhika na hilo, lakini ilimtuma mkuu wake wa ujasusi, William Burns, kuzuru eneo hilo kwa siku kadhaa, akielekeza ziara yake katika utawala wa Misri na umbile la Kiyahudi, hata kama alikuwa anakaa kati yao nchini Qatar. Hata hivyo, msisitizo ulikuwa katika kudhibiti uhusiano kati ya utawala wa Misri na umbile la Kiyahudi, hasa katika suala la Rafah. Hii inafanya kile Al-Arabi Al-Jadeed ilichochapishwa mnamo tarehe 8/5/2024 kuwa na kipengele kinachostahili kuzingatiwa:

(...Vyanzo vya kibinafsi vilifichua kwa Al-Araby Al-Jadeed kwamba uvamizi wa Rafah na kuwasili kwa gari za jeshi la "Israel" hadi mhimili wa Filadelfia, na hata kwenye lango la Misri la kivuko cha Rafah kutoka upande wa Palestina, zilikuja baada ya upande wa Misri kujulishwa juu yake, na kwa uratibu kamili wa Marekani... Chanzo hicho kilisema, “Mkurugenzi wa CIA William Burns alipanga operesheni hiyo na mkuu wa Mossad David Barnea, huku maongezi ya simu yakifanyika kati yake na Netanyahu, wakati ambapo alithibitisha hali ndogo ya operesheni hiyo.").

Kisha Marekani ilichochea kile ambacho baadhi ya watawala na vyombo kadhaa vya habari vilipongeza, yaani kwamba kulikuwa na mzozo kati ya Marekani na umbile Kiyahudi, na kwamba matumizi yake ya silaha za Marekani yalikuwa ni kinyume cha sheria. Blinken alisema hayo, lakini kwa njia ya kupindisha, ya kuzunguka, na ya udanganyifu, na haifichiki kwa wale wenye uelewa, kama ilivyoelezwa katika ripoti aliyowasilisha kwa bunge la Congress:

[Gazeti la Al-Khaleej: 11/5/2024 Washington - (AFP):

(Ripoti iliyosubiriwa kwa muda mrefu ya Wizara ya Mambo ya Nje mnamo siku ya Ijumaa ilisema kwamba “Israel” huenda ilikiuka kanuni za sheria za kimataifa katika matumizi yake ya silaha za Marekani lakini haikupata ushahidi wa kutosha kuzuia shehena.) Ripoti hiyo ilisema, (Ilitathmini kwa busara kwamba “Israel” “ilitumia silaha kwa njia zisizopatana na sheria za kimataifa za kibinadamu,” lakini Marekani “haikuweza kufikia mahitimisho madhubuti....” Ripoti hiyo ilisema kwamba (huku Marekani ikiamini kwamba “Israel” imechangia maafa yanayoendelea ya kibinadamu kwa njia ya "vitendo au kutotenda" kwake, haihitimishi kuwa mamlaka za "Israel" kwa makusudi "imepiga marufuku au kuzuia" utoaji na uhamishaji wa msaada huu ... nk.)] Ni wazi kwamba inabadilisha maneno ya kulaani na si kutolaani kwa wakati huo huo! Kwa kujali kuwaunga mkono Mayahudi, na kuwahadaa watawala katika nchi za Waislamu, na hata bila ya hadaa, wana ufahamu! Hii ni kuonyesha watu kana kwamba Marekani iko katika mzozo na umbile la Kiyahudi!

Enyi Waislamu:

Balaa iko kwa watawala hawa ambao wako katika kuhudumia makafiri wakoloni, hasa Marekani. Wanasema kile inachosema na kufanya kile wanachotaka. Wanashuhudia miili ya mashahidi kwa macho yao wenyewe, wanasikia mayowe ya watoto kwa masikio yao, na wanaona kuhama kwa watu na watoto wao na wanawake katika matukio ya kuvunja nyoyo. Watawala wameshuhudia yote haya. Yamefikia masikio na macho yao, lakini hayakuathiri uungwana wa Al-Mu'tasim (kivitendo)! Wamezuia majeshi yasiwanusuru ndugu zao huko Gaza Hashim. Badala yake, wamesimama na kutazama kile kilichokuwa kikitendeka, wakiwahesabu mashahidi na kuwaita “wafu” kwenye vyombo vyao vya habari. Walio bora zaidi miongoni mwao ni wale wanaopatanisha, kana kwamba ni kundi lisilofungamana na upande wowote kati ya umbile la Kiyahudi, adui wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na Waislamu wa Gaza wanaoshambuliwa katika kila shubiri ya Ukanda wa Gaza!

Enyi Askari katika Majeshi ya Waislamu:

Kungojea amri kutoka kwa watawala kupigana na Mayahudi na kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa ni sawa na mtu anayenyoosha mikono yake kwenye maji [kutoka mbali, akiyaita] ili yafikie kinywa chake, lakini hayatafika. Basi anzisheni harakati, nyinyi wenyewe, na Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi na Ummah utawafuata... Bila shaka mnasikia na kuona jinsi adui yenu anavyoushambulia kwa mabomu Ukanda wa Gaza ardhini, baharini na angani ili kuugeuza kuwa ardhi iliyoungua... kwa hiyo munashindwaje kuwanusuru ndugu zenu au kupigana?!

Enyi Askari katika Majeshi ya Waislamu:

Je! hakuna miongoni mwenu mtu mwenye hekima? Hususan katika ardhi ya Kinana (Misri) na Ash-Sham, atakayewaongoza askari na majeshi mengine yamfuate, wakipiga Takbira na Umma ukipiga nyuma yao katika ushindi wa Mwenyezi Mungu (swt).

[إِنَّا لَنَنْصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ]

Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watapo simama Mashahidi. [Ghafir: 51].

Imetosha sasa, Enyi Majeshi! Hakuna udhuru uliosalia kwa mwenye kutoa udhuru na hakuna udhuru kwa mwenye kulaani tu. Haitoshi kwenu kukaza meno yenu kwa hasira dhidi ya

[قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنْصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُؤْمِنِينَ]

Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini. [At-Tawbah: 14].

H. 5 Dhu al-Qi'dah 1445
M. : Jumatatu, 13 Mei 2024

Hizb-ut-Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu