Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Enyi Waislamu, Komesheni Machafuko Duniani kwa Kuwa na Tawakkul kwa Mwenyezi Mungu (swt) na Shariah Yake na Fanyeni Kazi kwa ajili ya Khilafah

(Imetafsiriwa)

Tangu kuvunjwa kwa Khilafah mwaka 1924, kila kona ya dunia imekuwa katika machafuko ya kuendelea. Hii ni licha ya kuwa kumekuwa na maendeleo katika teknolojia, matibabu, kilimo, jeshi, na inaonekana maendeleo katika siasa na katika kujenga haki sawa kati ya jinsi na jinsia. Tumehadaiwa katika kuamini kwamba mfumo ule ule unaotuambia kwamba hatuhitaji kutazama Quran na Sunnah (yaani, kutenganisha kanisa na dola), bali kwenda kwa mfumo uliobuniwa na mwanadamu (yaani, demokrasia) unaoegemezwa juu ya matamanio ya mwanadamu, na mfumo wa kiuchumi (yaani, ubepari) unaoegemezwa juu ya riba unaoweka wingi wa mali mikononi mwa wachache kuongoza mambo yetu yote ya maisha. Tunapaswa kukaa chini na kutafakari kwa nini machafuko haya yote yanatokea kwa kuendelea na kwa kila jaribio la "kuyasuluhisha", mambo yanazidi kuwa mabaya, au migogoro mipya inaundwa bila kujali ni kiasi gani cha maendeleo tunachoonekana kufanya. Kwa uchunguzi wa kina, inakuwa dhahiri kwamba migogoro hii siyo ya kimaumbile, bahati mbaya, au kiasili kutokea katika jamii, lakini kwa kubuniwa na wale waliochukua udhibiti wa dunia na kuulazimisha mfumo wa ubepari wa kisekula kutoka Mashariki hadi Magharibi.

Katika ulimwengu wa Kiislamu, ngao yetu ilipochukuliwa, tulilazimishwa kuishi chini ya madikteta wakatili, wafalme haramu, marais na mawaziri wakuu. Tulilazimishwa kuishi chini ya umaskini uliokithiri, ubadhirifu na wizi wa maliasili, kuvunjwa kwa taasisi za elimu na matibabu ambazo hapo awali zilikuwa vituo vya maendeleo na huduma bora za afya, kusambaratika kwa mahusiano kati ya mume na mke; wazazi na watoto kupitia kuanzishwa kwa ufeministi, ubinafsi, na LGBTQ+, vurugu za mara kwa mara, na janga la wakimbizi lisilokwisha ambalo limetusibu tangu tulipogawanywa katika dola za kitaifa. Walituondolea macho yetu ya jinsi ya kuendesha mambo yetu ya maisha kwa kubadilisha fahamu ya kibepari ya manufaa na madhara badala ya halali na haramu.

Hata hivyo, hata nchini Marekani, pamoja na nguvu zake zote, pesa, na sheria zinazobadilika kila mara zinazokusudiwa kuwa jumuishi na zilizoendelea; machafuko na migogoro kamwe haimaliziki. Licha ya kilio cha umma na maafisa wa serikali juu ya George Floyd, watu weusi nchini Marekani bado wanauawa na kufungwa kwa idadi kubwa zaidi kuliko jinsi nyengine yoyote, au kabila lolote. Licha ya ahadi za Biden na Wanademocrat kuwasaidia wale wanaotaka kuepuka umaskini na vurugu kuishi nchini Marekani, wahamiaji bado wamefungwa katika magereza wanaokabiliwa na uhamisho. Licha ya vuguvugu la kutetea haki za wanawake, wanawake nchini Marekani bado wanakabiliwa na ukosefu wa usawa wa kipato, bado wanafanywa kuwa ni vyombo, wanakabiliwa na unyanyasaji wa kijinsia uliokithiri, na wako katika hatari kubwa ya kuishi katika umaskini pamoja na watoto wao. Licha ya sheria za kumiliki bunduki, Marekani ina kiwango cha juu zaidi cha ghasia za bunduki miongoni mwa mataifa mengine tajiri ambazo zinazidi kuwa mabaya, kama inavyoonekana katika mojawapo ya matukio ya hivi punde ya ufyatuaji risasi shuleni ambapo mvulana wa miaka 6 alimpiga risasi mwalimu wake. Licha ya kuwa moja ya nchi tajiri zaidi duniani, uhaba wa chakula ni jambo la kawaida kwa Wamarekani milioni 34, pamoja na, wengine ambao hawana mifereji ya ndani, upataji elimu, huduma za afya, na maji safi! Licha ya kutangazwa kuwa kinara wa usawa na demokrasia, taifa lilishuhudia maasi maarufu ya mwaka 2021 ambayo yalifichua hali ya kutoridhika na migawanyiko iliyokuwepo ndani ya jamii.

Je, huyu ndiye tunayepaswa kumwangalia ili atuongoze? Je, hii sio ishara kwetu kwamba kuishi chini ya sheria zilizotungwa na mwanadamu hakutatuletea chochote isipokuwa machafuko na kiwewe?

Tunawezaje kuendelea kutazama demokrasia, ubepari na usekula ili kutatua matatizo yetu na ilhali Mwenyezi Mungu (swt) ametupa hukmu na ramani ya namna ya kuitabikisha kama ilivyowekwa na kipenzi chetu Mtume Muhammad (saw) alipoasisi dola mjini Madina? Ingawa inaweza kuonekana kana kwamba ni kazi kubwa, ni lazima tupate kishajiisho kutoka kwa Mtume wetu (saw) na Maswahaba (ra) pindi walipokabiliana ana kwa ana si tu na makabila madogo ya kipagani, bali na dola kuu za wakati huo; Warumi na Wafursi, ambao walikuwa bora zaidi kwa idadi na teknolojia ya kijeshi. Hata hivyo, kile ambacho Waislamu walipungukiwa nacho katika idadi na teknolojia, walikifidia kwa kitu chenye nguvu zaidi; Imani na Tawakkul kwa Mwenyezi Mungu (swt). Na Mwenyezi Mungu (swt) akawapa ushindi juu ya madhalimu wa zama zao. Waliitazama dunia kupitia kioo cha Uislamu na kilichowaongoza katika maamuzi yao ni kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu (swt). Hivi ndivyo walivyoweza kupiga hatua kubwa katika kueneza Uislamu kupitia utabikishaji wa Shariah na jihad fisabilillah kupitia dola ya Khilafah.

Ni lazima tuzingatie mafunzo haya na kama vile Maswahaba (ra) walivyofanya, tufikirie imani yetu kwa Mwenyezi Mungu (swt) na tukinai kwamba ni kupitia kumwamini Yeye pekee ndipo tutaweza kufanya mabadiliko ya kweli yanayohitajika kwetu kuleta utulivu na utulivu duniani. Kupitia Shariah, tuliyotumiwa na Muumba wetu, tunazo sheria kamilifu na zinazotosha kutatua mambo yetu yote na jaribio lolote la kutafuta hukmu kutoka kwa kitu chochote nje ya Shariah yake ni mtego wa Shetani ili atupoteze. Mwenyezi Mungu (swt) ametupa neema zake kwa kutukamilisha Dini yake na kutufanya kuwa mashahidi kwa wanadamu kama vile Mtume Muhammad (saw) alivyokuwa shahidi juu yetu.

[وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَـٰكُمْ أُمَّةًۭ وَسَطًۭا لِّتَكُونُوا۟ شُهَدَآءَ عَلَى ٱلنَّاسِ وَيَكُونَ ٱلرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًۭا]

“Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani, ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe ni shahidi juu yenu.” [Al-Baqarah:143]

Tunahitaji kujiangalia zaidi ya nafsi zetu kama watu binafsi na kukumbuka kwamba Mwenyezi Mungu (swt) aliituma Quran yake na Shariah yake kama rehma kwa wanadamu. Hili linauhitaji Umma wa Muhammad (saw) kujihuisha wenyewe kupitia imani yake thabiti kwa kurudisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kupitia kusimamisha tena Khilafah. Dhihirisho la kivitendo la Shariah bila shaka litatumika kama mwenge wa nuru na njia ya uokozi kwa ulimwengu ambao umezungukwa na giza na machafuko ya Urasilimali. Kupitia dola ya Khilafah, yenye kusimama nyuma ya Khalifa mwadilifu, Umma utakuwa tayari kutumia rasilimali zake zote kuupeleka Uislamu ulimwenguni.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Sarah Mohammed – Amerika

Fuatilia na Usambaze Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah

#EstablishKhilafah

#ReturnTheKhilafah

#TurudisheniKhilafah

#KhilafahBringsRealChange

#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي

أقيموا_الخلافة#

كيف_تقام_الخلافة#

#YenidenHilafet

 #HakikiDeğişimHilafetle

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu