Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan: Enyi Jeshi la Pakistan! Songeni kwa ajili ya Kuinusuru Gaza, kwa Kumtii Mwenyezi Mungu!

Televisheni ya serikali ya Pakistan ilisema mnamo 19 Machi 2025: “Pakistan inalaani vikali mashambulizi ya anga ya Israel.” Hivi ndivyo watawala wa Pakistan walivyolaani hujuma ya Mayahudi na jinai zake zinazoendelea dhidi ya Ukanda wa Gaza! Bila kusonga askari au kuinua silaha! Enyi Maafisa wa Jeshi la Pakistan! Je, mnawafuata watawala wanaofuata sera za dola za kikoloni na kuuweka utiifu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake (saw) nyuma ya migongo yao? Wanajifanya kana kwamba hawaegemei upande wowote huku ndugu zetu huko Palestina wakiuawa na kuangamizwa! Watawala hawa wanalinda maslahi ya dola  za kiadui huku mauaji yakifanywa dhidi ya watu wa Palestina. Utiifu wenu kwao hautakuepusheni na fedheha ya dunia na adhabu ya Akhera, na mutajuta wakati majuto hayatafaa kitu.

#Time4Khilafah

Imetayarishwa na: Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Ijumaa, 21 Ramadhan 1446 H sawia na 21 Machi 2025 M

#طوفان_الأقصى

#الجيوش_إلى_الأقصى

#الأقصى_يستصرخ_الجيوش

#AksaTufanı

#OrdularAksaya

#ArmiesToAqsa

#AqsaCallsArmies

Kwa Maelezo zaidi, Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan

 Tovuti Rasmi: Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan

 Facebook: Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan

Twitter: Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.